Dkt. Ndugulile awaasa Wananchi kushiriki kikamilifu shughuli za Maendeleo

0
27

Naibu Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsioa,Wazee na Watoto Dkt.Faustine Ndugulile amewataka wananchi kutumia nguvu kazi yao katika ujenzi na uboreshaji wa Zahanati katika Wilaya zao kuliko kupeleka pesa nyingi kwa wakandarasi.

Dkt.Ndugulile ameyasema hao wilayani hapa wakati wa ziara ya kikazi ya kukagua shughuli za utoaji huduma za afya na kutathimini shughuli za maendeleo ikiwemo ya upanuzi wa miundombinu zikiwemo ya Zahanati

Alisema kutumia nguvu kazi zao itasaidia kwa kiasi kikubwa kupunguza gharama ambazo zingeweza kujitokeza kama wangetoa tenda hiyo kwa wakandarasi.”Nyinyi ndio wasimamizi wakuu wa shughuli hizi na mkiharibu tutakuja kuwalaumu nyinyi

Aidha,alisema Serikali imetoa shilingi milioni 400 kwa ajili ya kuboresha miundombinu ya huduma za afya nchini kwa upande wa uzazi wa dharura ikiwemo upasuaji, wodi ya wazazi,maabara ,wodi ya watoto pamoja na nyumba ya mtumishi kwenye vituo vya afya ambapo ujenzi huo unaanza mara moja

Kwa upande mwingine Dkt. Ndugulile ameendele kuwatoa hofu wananchi juu ya hali ya upatikanaji wa dawa, huku akiwasisitiza wananchi wasiuziwe dawa zozote muhimu kwani hali ya upatikanaji wa Dawa ni nzuri maeneo yote na sasa ni wastani wa asilimia 80.

Katika kituo cha Afya Kanoge, bajeti ya dawa imeongezeka kutoka Milioni 300 mpaka Bilioni 2.5, kwahiyo dawa tunazo za kutosha, hivyo hatutarajii kuona mtu aje hapa aambiwe akanunue dawa sehemu nyingine, wamenithibitishia waganga wangu asilimia 90 ya dawa muhimu zipoaliendelea Dkt. Ndugulile

Wakati huo huo Dkt. Ndugulile amesisitiza watumishi wa afya juu ya utunzaji wa kumbukumbu za dawa katika stoo ya madawa ikiwemo kuweka za kujua idadi za dawa zilizoingia na kutoka pamoja na utunzaji wa takwimu za mahudhurio ya wagonjwa wa kila siku, jambo linalopunguza. 

ufanisi katika kazi.

Hata hivyo Dkt. Ndugulile amemtaka Mganga Mkuu wa Manispaa ya Mpanda Dkt. Mahenge kuanzisha ofisi ya kushughulikia malalamiko ya watu pindi wanapokutana na changamoto wakati wakipata huduma katika Kituo hicho cha Afya.

Naye Mganga Mkuu wa Mkoa wa Katavi Dkt. Yahaya Hussein wakati akiwasilisha taarifa ya Mkoa alisema kuwa Mkoa wa Katavi unakabiriwa na uhaba mkubwa wa watumishi wa kada ya Afya hali inayopelekea changamoto kubwa katika utoaji wa huduma kwa wananchi.

Hadi kufikia Septemba 2017 Mkoa wa Katavi una jumla ya watumishi 693 sawa na asilimia 28 kati ya watumishi 2,437 wanaohitajika, kati ya hao 19 ni watumishi ngazi ya Mkoa na 674 ngazi ya Serikali za mitaa, kwa ujumla Mkoa wa Katavi una jumla ya upungufu wa watumishi 1,744” Alisema Dkt. Hussein.

Dkt. Yahaya Hussein aliongeza kuwa Mkoa unaendelea kuzisimamia Halmashauri kuhakikisha zinatenga bajeti kwa ajili ya kuwakatia kadi za Afya ya Jamii (CHF) wazee ili kuendelea kupata Huduma za Afya kwa urahisi katika maeneo yao.

Mpaka kufikia Mwezi Septemba 2017 jumla ya wazee 19,248 wametambuliwa, na kati ya hao jumla ya wazee 1,807 sawa na asilimia 9.4 wameshapatiwa kadi za CHF katika Halmashauri zote za Mkoa wa Katavi.

Na WAMJW. KATAVI.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here