Dk.Kigwangalla: Kila Mwaka watu 60,000 wanakufa kwa Malaria nchini

0
391

Kila ifikapo Aprili 25 ya mwaka Duniani kote Mataifa yanaadhimisha juu ya ugonjwa Malaria ambao umeweza kusababisha vifo vya watu wengi Duniani kote.

Kupitia kurasa za mtandao wa Kijamii wa Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee na Watoto. Mh. Dkt. Hamisi Kigwangalla amewataka watanzania kujikinga na Malaria hasa watoto wadogo ambao ikiwemo kwa njia ya kujikinga kwa kutumia chandarua.

Miongoni mwa takwimu alizoweka ni pamoja na : “Ili kuokoa watoto dhidi ya malaria, jitihada za kinga ya maambukizi zimetupelekea kugawa net zenye dawa zaidi ya milioni 10 toka 2009!” ameandika Dk. Kigwangalla kupitia akaunti yake ya twitter.

Na kuongeza kuwa: “Katika kila watu 100 wanaokufa kwa #Malaria, watoto chini ya miaka mitano ni 80. Kila mwaka wanakufa watu 60,000 kwa malaria hapa nchini!” alieleza Dk. Kigwangalla kupitia akaunti yake hiyo ya twitter.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here