Dk.Kigwangalla “Watoto wa kike pendenimasomo ya Sayansi, ICT”

0
242

Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee na Watoto. Mh. Dkt. Hamisi Kigwangalla amewahimiza wasichana nchini kuwa na utayari wa kupenda kusoma masomo ya Sayansi ilikuendana na masuala ya ICT.

Dkt. Kigwangalla ameyasema hayo mapema leo Aprili 27.2017, Jijini Dar e Salaam wakati wa kukabidhi vyeti kwa wasichana waliokuwa wakipatiwa mafunzo maalum ya ICT, mafunzo yaliyoendeshwa na d Lab Tanzania.

Awali Dkt. Kigwangalla aliwahiza wasichana hao kuendelea kupenda masomo hayo ya Sayansi  ili waweze kuendeleza vipaji vyao katika sekta ya ICT na kufikia malengo yao ya baadae ambapo ameweza kuwatia moyo wasichana  hao waendelee kujifunza na wasiogope masomo  hayo ya Sayansi na na wawe wabunifu kwani bado wanahitajika kwa dunia ya sasa.

Mafunzo hayo yalitolewa na d Lab Tanzania yamewahusisha Wasichana waliopo mashuleni na waliomaliza shule ambapo  na kupatiwa mafunzo maalum  katika ICT na hii leo ilikuwa ni kilele chamafunzo hayo ambapo pia ni siku ya Wasichana Kimataifa katika ICT.

Wasichana washiriki wakiwa katika mafunzo hayo wakati wa kuwasilisha mada

Baadhi ya wasichana wakifuatilia mafunzo hayo

Mafunzo hayo yakiendelea

Mafunzo hayo yakiendelea

Mmoja wa Wasichana akiwasilisha mada namna alivyoweza kutengeneza program katika mafunzo hayo ya ICT

Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee na Watoto. Mh. Dkt. Hamisi Kigwangalla akifuatilia mafunzo hayo yaliyokuwa yakiwasilishwa na mmoja wa Wasichana (Hayupo pichani)

Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee na Watoto. Mh. Dkt. Hamisi Kigwangalla akikabidhi vyeti kwa washiriki Wasichana  wa mafunzo ya ICT yaliyoandaliwa na d Lab Tanzania  

Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee na Watoto. Mh. Dkt. Hamisi Kigwangalla akikabidhi vyeti kwa washiriki Wasichana  wa mafunzo ya ICT yaliyoandaliwa na d Lab Tanzania  

Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee na Watoto. Mh. Dkt. Hamisi Kigwangalla  akipata picha ya pamoja na baadhi ya washiriki pamoja na waandaaki wa mafunzo hayo ya maalum ya ICT kwa Wasichana  yaliyoandaliwa na d Lab Tanzania.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here