Taasisi ya Sanaa Bagamoyo kuzindua mafunzo kwa Vijana 27 kutoka Mbeya kwa ufadhili wa Tulia Trust

0
107

Taasisi ya Sanaa na Utamaduni Bagamoyo (TaSUBa) kwa kushirikiana na Tulia Trust  wanatarajia kuzindua rasmi mafunzo maalumu ya Sanaa kwa vijana 27 kutoka Mkoani Mbeya, tukio ambalo linatarajiwa kufanyika siku ya Jumamosii ya Aprili 29.2017, ndani ya ukumbi wa maonyesho wa TaSUBa, wilayani Bagamoyo ambapo Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Dkt.Tulia Ackson Mwansasu (Mb.) anatarajia kuwa mgeni rasmi.

Vijana hao 27 kutoka Wilaya za Rungwe, Busokelo na Kyela, Mkoa wa Mbeya wamepata ufadhili huo kutoka kwa Mh. Dkt. Tulia ambaye ni mwanzilishi wa Tulia Trust, ambapo ameweza kuwafadhili vijana hao ilikupata elimu maalum ya Sanaa na Utamaduni  ambapo ameweza kuwagharamia mafunzo  ikiwemo pamoja  na kulipia ada za masomo, chakula, malazi na usafiri kwa muda wote wawapo Chuoni hapo.

Wanafunzi hao tayari wapo Chuoni hapo wakiendelea na mafunzo hayo ya Sanaa na Utamaduni yanayotolewa na wakufunzi mabingwa na mahiri wa taasisi hiyo ya Sanaa ambayo ni kubwa kwa hapa nchini na Ukanda wa Afrika Mashariki.

Mafunzo hayo yamegawajika katika awamu mbili; awamu ya kwanza ina jumla ya vijana 20 ambao tayari wameishaanza mafunzo chuoni hapo ambapo  watapata mafunzo maalumu kwa muda wa miezi miwili. Mafunzo hayo yatahusisha kujifunza uchezaji ngoma za asili ya Tanzania, ngoma za ubunifu, muziki wa asili ya Tanzania, uigizaji, matumizi ya jukwaa na maleba.

Kwa awamu ya pili itahusisha vijana 7 ambao watapata mafunzo katika ngazi ya stashahada (diploma) na Astashahada (certificate) katika fani za Sanaa za maonyesho na ufundi (performing and visual arts).

Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Dkt.Tulia Ackson Mwansasu (Mb.) ambaye atakuwa mgeni rasmi katika tukio hilo.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here