Wafanyakazi wa Zantel watembelea Polisi Oysterbay kuadhimisha siku ya Afya na Usalama mahali pa kazi Duniani

0
103

Wafanyakazi wa Kampuni ya Zantel wametembelea kituo cha Polisi Oysterbay Jijini Dar es Salaam katika kuadhumisha siku ya Afya na Usalama mahala pa kazi Duniani.

Katika ziara hiyo  fupi katika kituo hicho cha Polisi cha Oysterbay,  mwishoni mwa juma ambapo wafanyakazi hao waliambatana na  Meneja wa Afya, Ulinzi na Usalama wa Kampuni ya Mawasiliano ya Zantel, Nashon Mudala aliweza kufafanua kuhusu alama muhimu za usalama kwa wafanyakazi wa Zantel ambazo wanatakiwa kuzizingatia pindi wanapokuwa kazini .

Ziara hiyo ilifanywa na wafanyakazi hao mara baada ya kukamilisha matembezi mafupi ya kuadhimisha siku ya Afya na Usalama mahali pa kazi duniani. Wafanyakazi wengine waliokuwa katika tukio hilo ni pamoja na  Mkuu wa Sheria na Manunuzi Zantel, Rehema Khalid na Afisa Mkuu wa masuala ya kiufundi Zantel, Larry Arthur.

Meneja wa Afya, Ulinzi na Usalama wa Kampuni ya Mawasiliano ya Zantel, Nashon Mudala (aliyesimama kulia) akifafanua kuhusu alama muhimu za usalama kwa wafanyakazi wa Zantel (Hawapo pichani) ambazo wanatakiwa kuzizingatia pindi wanapokuwa kazini. Katikati ni Kamanda wa Polisi wa kikosi cha Usalama barabarani wa Wilaya ya Kinondoni, ACP Theopista Mallya, Mkuu wa Sheria na Manunuzi Zantel, Rehema Khalid (Kushoto) na Afisa Mkuu wa masuala ya kiufundi Zantel, Larry Arthur.

Kamanda wa Polisi wa kikosi cha Usalama barabarani wa Wilaya ya Kinondoni, ACP Theopista Mallya akizungumza na wafanyakazi wa Zantel walipomtembelea katika kituo cha Polisi cha Oysterbay jijini Dar es salaam mwishoni mwa wiki mara baada ya wafanyakazi hao kukamilisha matembezi mafupi ya kuadhimisha siku ya Afya na Usalama mahali pa kazi duniani. Kulia ni Afisa Mkuu wa masuala ya kiufundi Zantel, Larry Arthur.

Askari wa Usalama barabarani, Wilaya ya Kinondoni S/SGT Rehema (kulia) akieleza kuhusu masuala ya usalama barabarani kwa wafanyakazi wa Zantel katika kituo cha Polisi cha Oysterbay jijini Dar es salaam mwishoni mwa wiki mara baada ya wafanyakazi hao kukamilisha matembezi mafupi ya kuadhimisha siku ya Afya na Usalama mahali pa kazi duniani. Kushoto ni Kamanda wa Polisi wa kikosi cha Usalama barabarani wa Wilaya ya Kinondoni ACP Theopista Mallya na Afisa Mkuu wa masuala ya kiufundi Zantel, Larry Arthur.

Kamanda wa Polisi wa kikosi cha Usalama barabarani wa Wilaya ya Kinondoni, ACP Theopista Mallya akiwaonyesha wafanyakazi wa Kampuni ya Mawasiliano ya Zantel picha iliyotumwa na wadau wa usalama barabarani inayoonyesha matumizi mabaya ya barabara yanayofanywa na madereva wazembe. Wafanyakazi hao walifanya ziara katika kituo cha Polisi cha Oysterbay jijini Dar es salaam mwishoni mwa wiki mara baada ya kuhitimisha matembezi mafupi ya kuadhimisha siku ya Afya na Usalama mahali pa kazi duniani. Kushoto ni Mkuu wa Sheria na Manunuzi Zantel, Rehema Khalid.

Kamanda wa Polisi wa kikosi cha Usalama barabarani wa Wilaya ya Kinondoni, ACP Theopista Mallya (wa pili kushoto) akimsikiliza Mkuu wa Kitengo cha Intaneti na Simu wa Kampuni ya Mawasiliano Zantel, Hamza Zuheri  alipotembelewa na wafanyakazi wa Kampuni hiyo katika kituo cha Polisi cha Oysterbay jijini Dar es salaam mwishoni mwa wiki. Wafanyakazi hao walifanya ziara hiyo mara baada ya kuhitimisha matembezi mafupi ya kuadhimisha siku ya Afya na Usalama mahali pa kazi duniani.

Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Mawasiliano ya Zantel, Benoit Janin akizungumza na wafanyakazi wa Zantel mara baada ya wafanyakazi hao kuhitimisha matembezi mafupi ya kuadhimisha siku ya Afya na Usalama mahali pa kazi duniani. Hafla hiyo iliyofanyika katika makao makuu ya Kampuni hiyo Msasani jijini Dar es salaam mwishoni mwa juma.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here