Msaga Sumu,Shilole,Dulla Makabila kupiga shoo ndani ya JM Manzese Mei 6 Dar

0
203

Wasanii  wa muziki wa kizazi kipya na muziki wa Singeli, Msaga Sumu, Dulla Makabila, Shilole, Edu Boy na Pink, Jumamosi Mei 6,  watapanda kwenye jukwaa moja katika onesho maalum na  Silawadu, lityakalofanyika kwenye Ukumbi wa JM Manzese Jijini Dar es Salaam.

Mratibu wa onyesho hilo Soud Brown, alisema kuwa onyesho hilo la maalum la kipekee limepelekwa Mazense kwa lengo la kutoa burudani kwa wakazi wa eneo hilo.

Alisema kuwa wana amini kila msanii waliyemchukua atatoa  burudani ya aina yake kwa wakazi wa mazense, ambao  hawajawahi kupata muunganiko huo.

Brown alisema kiuwa onyesho hilo litaanza majira ya saa 2, usiku  kwa kila msanii kutoa burudani kwa muda wa kutosha.

“Kama mratibu nina amini kila mpenzi atakayepata nafasi ya  kuja kwenye onyesho letu atapata burudani ya kutosha kutoka  kwa kila msanii tuliyemchukua maana wote ni wasanii wazuri na  wana nyimbo zinazopendwa na kila mpenda muziki hapa nchini”alisema Brown.

Msanii Shilole

Msanii Dulla Makabila

Msanii Msaga Sumu

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here