Tahadhari Video za Ngono!!

1
7185

Elewa kwamba XVIDEOS ni video za ngono ambazo pia hujulikana kama Mikanda ya X, na XPICTURES ni picha za uchi zilizopigwa na watu mbalimbali kote ulimwenguni ambapo nyingi kat yazo hupigwa na wanawake.

Sasa leo nataka kukujuza jambo hili, ya kuwa Amin usiamin ndugu yangu ukweli ni kwamba si video zote za ngono huchezwa na watu wa kawaida, zipo ambazo huchezwa na ‘evil spirits’ kama vile majini ambayo huchukua umbo la mtu na kuonekana kama mtu wa kawaida.

Nadhan wote tunajua ‘majini’ ni roho na roho hizo zinauwezo wa kujivika maumbo ama miili ya vitu mbalimbali ikiwemo miili ya wanyama au hata miili ya wanadamu, jambo ambalo huweza kufanywa pia na wachawi wa viwango vya juu.

Kumbe basi unaweza kutazama video hizo au picha hizo za uchi ukizan unawatazama wanadamu wa kawaida kumbe ukawa unatazamana live na majini yaliyochukua shape za watu.

Na kwa kutazama huko ndipo unakuwa umefungua mlango kwa roho hizo kukuingia wewe na kukutumikisha kadri zipendavyo. Na roho hizo za kishetan zinapomwingia mtu humfanya kuwa mtumwa wa video hizo.

Watu wengi wamekuwa wakitazama video hizo kwa kisingizio cha kujifunza ‘style’ mbalimbali za ufanywaji wa tendo hilo! Je ni kweli nuru yaweza kujifunza kitu chema katikati ya giza?

Au ni mkristo yupi kati yetu anayeweza kutuambia ni wapi Adamu na Eva walipojifunza ama kutazama ufanywaji wa tendo hilo hata wakawazaa Kain na Abeli? Ndio maana leo hii wapo wengine wenye ndoa zao lakini hawapati tena msisimko wa mwili kwa kuwatazama wake zao hadi pale watakapotizama video hizo au picha hizo.

Je huu sio utumwa? Lakini pia sote tunajua ya kuwa ukimtizama tu mwanamke kwa kumtamani tayari unakuwa umezini nae rohoni mwako, je waweza kweli kuikwepa dhambi hii pale unapotazama picha na video hizo chafu? Wengine wameishia kujifunza ufanywaji wa tendo hilo kinyume cha maumbile yaaani ‘anal sex’ kisha kuwalazimisha wenzi wao kufanya kwa kupitia njia hiyo

 je Mungu hakukataza mambo hayo? Wapo pia wafanyao homosexual (yan watu wa jinsia moja) au group sex (yan mwanaume m1 akiwa na wanawake zaid ya m1 au mwanamke m1 akiwa na wanaume zaid ya m1).

Je twaweza kujifunza kitu gan chema toka kwa watu hao wafanyao mambo hayo ya sodoma na gomora? Au uliwahi kuona video hata 1 kati ya hizo wachezaji wake wanaanza kwa sala ya kumwomba Mungu na kisha wakahitimisha japo hata kwa maombi mafup? Ajabu utumwa huo leo umewafanya watu wengine kuficha video hizo na picha hizo kwenye laptop zao, desktop, ipad au hata kwenye simu zao na kulock mafile hayo kwa kuyawekea password au majina ya kujua wao, lakini je unapofanya hvyo unakuwa unamficha nani hasa?

Je unadhani wakati ‘unahide mafolder’ hayo Mungu huwa hakuoni? Ni kwel unaweza kuwaficha wanadamu lakini  je waweza pia kumficha hata Mungu wako?

Neno la Mungu katika Warumi 1:28-32 linasema watu wanayajua mambo yote maovu yawapasayo hukumu lakini pamoja na kuyajua kwao bado wanayafanya mambo hayo na wale wasiyoyafanya wanakubaliana na wale wayafanyayo.

Mfano pengine kweli wewe hufanyi ‘Anal sex’ ,’group sex’ au hufanyi kabisa zinaa lakini unakubaliana na wafanyao zinaa kwa kuwatazama au hata kwa kuwahifadhi kwenye PC au simu yako, je hujui kwa kufanya hivyo unakuwa huna tofauti yeyote na wao?

Pole sana ndugu yangu kama na wewe u miongon mwa watu wengi wanaotumikishwa na roho hizo chafu. Cha kufanya: We fanya toba ya kweli na umwombe Mungu msamaha huku ukikusudia kuacha, kisha futa na udelete kabisa video ama picha hizo mahali popote ulipozihifadhi then mwombe Mungu akusaidie kuikimbia zinaa and lastly tafuta watu wa maombezi wakuombee maombi ya deliverance ili ufunguliwe toka katika vifungo hivyo ulivyofungwa na roho hizo bila ya wewe kujua.

Kumbuka “Aonywae mara nyingi akishupaza shingo, atavunjika ghafla wala hatapona tena (Mithali 29:1)

Kutoka WhatsApp Group.

 

1 COMMENT

  1. Hapo najua umetumia imani kuwaaminisha watu unacho kiamini lengo ni moja tu kuwakutanisha watu na mungu kwa kutumia uongo hakuna uthibitisho wowote kuwa jini laweza ku shoot video

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here