Waziri Ummy Mwalimu: Watoto majeruhi wa ajali ya Karatu wanaendelea vizuri

0
128

Hayo yqmesema leo na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto  Ummy Mwalimu  alipotembelea watoto wa shule ya Lucky Vicent ambao ni majeruhi wa ajali iliyotokea katika eneo la Rhotia Marera, Wilaya ya Karatu, Mkoani Arusha, na kupelekea vifo vya watoto 33 na watumishi 3.

Akiwa nje ya wodi ya wagonjwa mahututi walipolazwa watoto hao katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Arusha (Mount Meru), Waziri Mwalimu aliuhakikishia umma wa watanzania kuwa majeruhi hao wanaendelea vizuri; na kuwa tayari Wizara imeshapeleka Madaktari bingwa Watatu kutoka Taasisi ya Mifupa Muhimbili (MOI) ili wasaidiane na Madaktari wa Mount Meru na wale madaktari watalii kutoka shirika la STEMM Marekani.

Waziri Ummy amewahakikishia wazazi, walezi, ndugu na jamaa wa majeruhi kuwa Wizara ya Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto, itahakikisha watoto wetu wanapata matibabu sahihi ili waweze kurejea shule kuendelea na masomo.

Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mh. Ummy Mwalimu  akimjulia hali mmoja wa watoto wanaopatiwa matibabu katika Hospitali hiyo ya Mt. Meru, Kulia ni Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Mt. Meru,  Dkt. Jackline Uriyo.

 

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here