Beki kisiki wa timu ya Taifa Uganda na Tusker FC ya Kenya Batambuze asaini Singida United

0
315

Tayari Klabu ya Singida United ya Mkoani Singida imefanikiwa kunasa saini ya beki kisiki wa timu ya  Taifa ya Uganda ambaye pia anachezea Tusker FC  ya Kenya,  kinda, Shafik Batambuze (Pichani).

Batambuze ni miongoni mwa wachezaji mahiri katika timu yake ya Taifa ya Uganda na Klabu yake hiyo ya Tusker FC ya Kenya, ambapo mwaka huu pia ameweza kung’ara katika safu ya ulinzi na timu yake ya Taifa ya Uganda kwenye michuano ya AFCON 2017, nchini Gabon.

Habari zimebainisha kuwa, Batambuze amekubali kuanguka saini ya miaka miwili na Singida United FC.

Kwa mujibu wa mjumbe wa Kamati ya usajili ya Singida United Fc, Festo Sanga  ambaye yupo nchini Kenya kushughulikia usajili wa mchezaji huyo, amesema kuwa baada ya mchezaji huyo kwa sasa tayari wamefikisha idadi wachezaji wa kigeni wanne ambao wanatakiwa kikanuni za Ligi Kuu.

Miongoni mwa wachezaji wengine wa kigeni waliokwisha kuwasajili ni pamoja na Wazimbabwe watatu ambao ni Elisha Muroiwa, Wisdom Mtasa na Twafaza Kutinyu na Mganda huyo akimalizia kufunga dimba,  kwa wachezaji wa Kimataifa.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here