Meya Arusha, Waandishi wa Habari washikiliwa wakiwa Lucky Vicent Arusha

0
162

Kutoka Jiji la Arusha Zinaeleza kuwa Waandishi wa Habari 10 kutoka vyombo mbalimbali vya Habari wamekamatwa na Jeshi la Polisi baada ya kukutwa wakiwa wamefanya mkusanyiko ndani ya viunga vya shule ya Lucky Vicent iliyopo Jijini Arusha ambapo pia imeelezwa Mstahiki Meya wa Jiji hilo nae amekamatwa.

 Dulu za habari zinaeleza kuwa kukamatwa kwao ni baaada ya kufanya mkutano bila taarifa huku baadhi ya  Wanahabari  hao ni pamoja na Godfrey Thomas ayo tv, .Alphonce kusaga Triple A,Filbert Rweyemamu mwananchi, Husein Tuta Itv, .Joseph Ngilisho Sunrise radio,Geofrey Steven Radio 5, Janeth Mushi Mtanzania. Zephania Ubwani The Citizen, Elihuruma Yohani mwakilishi wa  Tanzania Daima, Idd uwesu Azam Tv.    

BongoNews1 bado inaendelea kusaka taarifa zaidi kutoka Jijini Arusha na tutawajuza hivi punde. Awali imeelezwa kuwa, Mstahiki Meya wa Jiji la Arusha, Kalist Lazaro pamoja na wadau wengine walichanga pesa kiasi cha shilingi milioni 28 waliamua

kukabidhi pesa hizo mchana wa leo kwa wahusika moja moja baada ya kuona sintofahamu zilizotokea kwenye michango ya wafiwa siku za karibuni, lakini ghafla Polisi wakatokea na kuwaambia walifanya mkusanyiko usio rasmi na kuwakamata.

      

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here