Alfred Lucas: Kuvunjika koleo sio mwisho wa uhunzi

0
146

Muda mfupi mpira baina ya timu ya Vijana ya Serengeti Boys ya Tanzania umemalizika huku tukipoteza kwa kufungwa bao 1-0 na Niger. kwa hatua hiyo, tumeshindwa kusonga mbele na na safari yetu kuishia hapo.

Hata hivyo, Msemaji wa Shirikisho la Soka Nchini (TFF) Alfred Lucas ambaye yupo nchini Gabon, ameweza kuandika ujumbe huu:

“Tujipange sasa kwa: 1.Qualifiers za 2019 Afcon U20  zinafanyika mwakani mwezi June

2.Afcon U17 finals zinafanyika Tanzania mwaka 2019. Serengeti Boys hii sasa inakuwa Ngorongoro Heroes na ikisha pumzika itaingia tena kambini.

U15 walioko Alliance school Mwanza wanakuwa Serengeti Boys wapya. Hakuna muda wa kusononeka ni kuchapa kazi tu.Kikubwa tunaandaa Taifa stars ya kwenda World cup 2026 na qualifiers zake zitaanza mwaka 2024.” Ameandika Alfred Lucas andiko lake katika mitandao ya kijamii.

 

Baada ya mchezo huo wa leo usiku Mei 21-2017, ambao Serengeti Boys imelala bao 1-0.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here