Prof. Ndalichako aahidi kumsaidia Zawadi Msigala mlemavu wa viungo aliyeripotiwa na TBC

0
97

Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Profesa Joyce Ndalichako ameahidi kumsaidia mwanafunzi mwenye ulemavu wa viungo anayeandika kwa komputa kutumia miguu Zawadi Msigala ambaye TBC ilirusha taarifa zake wiki iliyopita.

Profesa Ndalichako ametoa ahadi hiyo katika kipindi cha Jambo Tanzania kinachorushwa na TBC.

Zawadi Msigala mwenye umri wa miaka 18 alichaguliwa kujiunga na shule ya sekondari Songea mkoani Ruvuma ingawa alishindwa kuendelea na masomo kutokana na kukosekana miundombinu rafiki kwa hali aliyonayo.

Kijana huyo kwa sasa yupo nyumbani akisubiri kutumia nyumba wanayoishi mapacha walioungana Maria na Consolata iliyojengwa na serikali shuleni Udzungwa.

kutoka: tbchabari

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here