Unahitajika msaada wa haraka kwa Binti Mariam Mwema kwenda kutibiwa India

0
168

BONGONEWS  tunaungana na wadau wote,watanzania wote katika kampeni ya kuhamasisha watu kumsaidia Mariam Mwema anayesumbuliwa na tatizo la tumbo. Mariam Ibrahim Mwema mwenye umri wa miaka 16, tu hadi sasa ameshafanyiwa Operesheni 10, akiwa  chini ya umri wa miaka 18, ili kusaidia unafuu wa maumivu anayoyapata Mariam, tukiwa Mabalozi, tunaungana katika kuhamasisha Watu mbalimbali kujitokeza kufanikisha michango ya haraka ili akatibiwe nje ya nchi, India kama alivyoshahuriwa na Madaktari wa hapa Tanzania. Asanteni sana.

Maelezo ya  Mwalimu Mlezi wa Binti Mariam.

“Kuna mwanafunzi wetu anaitwa Mariam Ibrahimu Mwema wa shule ya sekondari Kawe Ukwamani, kidato cha 4 mwenye umri wa miaka 16 tu ana matatizo makubwa ya tumbo. Alifanyiwa opereshen ya kwanza  akiwa darasa la 3. Baadae  upasuaj uliendelea takriban mara 9.

Kwa sasa hali yake kiafya imezorota tena baada ya kuimarika katika miezi 2i iliyopita kufuatia operation aliyofanyiwa pale Muhimbili ambayo Ilikuwa ni operation ya kumi (10) kwa Mariam ambaye ni binti mwenye umri chini ya miaka 18’.                   

Hali ya Mariam kwa sasa si nzuri anaumwa sana na hata kukaa  hawezi, tumbo limevimba tena na zaidi familia yake haina uwezo na uchumi wao ni duni.

“Tunawaomba wadau kwa kila mmoja wetu afikirie nini anachoweza kumfanyia  Mariam kunusuru kiza  kinene cha mustakabali wake kimaisha. Kiukweli wazazi wake wamefikia hatua ya kutokujua hatma ya mtoto wao kipenzi.                     

Wazazi hawana kitu imebaki ni kumtazama tu, mtoto analia wazazi wanalia. Inaumiza sana pale Mariam anapokuambia japo kama ingekuwa inawezekana basi yeye akupatie nafsi yake nawe umpatie yako japo kwa masaa 2 ( dakika 120) japo naye apumzike maumivu kwa muda huo”.

  Gharama  kutibwa  India zinazohitajika ni Dola 8000

Kwa mujibu wa maelezo ya Madaktari wa hapa nchini wa  TMJ, SANITAS na Shree Hindu Mandal, wameshahuri msaada unaohitajika kwa sasa ni Matibabu ya haraka nje ya nchi ikiwemo India kwa mujibu wa maelezo ya madaktari hao.

Kwa msaada wa madaktari hao wamebainisha kuwa, gharama za matibabu pamoja  na gharama nyingine kuwa ni takriban dola elfu nane ( 8000) za marekani. Ameeleza Mwalimu Ajuaye Yusuph ambaye ni  Mwalimu wa Shule ya Ukwamani anaposoma Mariam.

Kwa hatua hiyo, wadau mbalimbali wakiwemo viongozi wa Serikali, dini, wafanyabiashara na wengine wengi wanahitajika kujitokeza kwa hali na mali kumsaidia Mariam.

Kwa msaada zaidi ikiwemo kumchangia ama kumsaidia Mariam, unaweza kuwasiliana na Mwalimu Mlezi  wa Mariam Ibrahim Mwema ambaye ni Mwalimu wa shule ya Ukwamani, kwa namba- 0683916283 au Namba ya Mama Mzazi wa Mariam-0685379888.

Majibu ya watalaam

Mariam Ibrahimu Mwema wa shule ya sekondari Kawe ukwamani akiwa amelala Kitandani,anahitaji msaada wa Watanzania wote kwa sasa. Kwa msaada zaidi ikiwemo kumchangia ama kumsaidia Mariam, unaweza kuwasiliana na Mwalimu Mlezi  wa Mariam Ibrahim Mwema ambaye ni Mwalimu wa shule ya Ukwamani, kwa namba- 0683916283 au Namba ya Mama Mzazi wa Mariam-0685379888.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here