Soma hapa Muhtasari wa taarifa ya Kamati Maalum ya Kuchunguza MAKINIKIA

0
89

MUHTASARI

MUHTASARI TAARIFA YA KAMATI MAALUM ILIYOUNDWA NA RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA MHE. DKT. JOHN POMBE MAGUFULI KUCHUNGUZA MCHANGA ULIO KATIKA MAKONTENA YENYE MCHANGA WA MADINI (MAKINIKIA) YALIYOPO KATIKA MAENEO MBALIMBALI NCHINI TANZANIA.

Utangulizi Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Joseph Magufuli aliteua Kamati maalum ya wajumbe wanane kuchunguza aina na viwango vya madini yaliyomo kwenye mchanga wa madini uliomo ndani ya makontena yaliyozuiliwa na Serikali kusafirishwa nje ya nchi.

Uteuzi huo ulifanyika tarehe 29/03/2017. Wajumbe wa Kamati hiyo wana taaluma katika fani za jiolojia, kemia, uhandisi kemikali na uhandisi uchenjuaji madini. Chimbuko la kufanyika kwa uchunguzi huu ni kutokana na ukweli kuwa viwango vya madini yaliyopo kwenye makinikia havijulikani, na hata mikataba ya uchenjuaji makinikia haipo wazi. Hali hii inaleta hisia kuwa nchi inaibiwa na hainufaiki na uchimbaji wa madini.

Katika kutekeleza uchunguzi huu, Kamati iliongozwa na Hadidu za Rejea zilizoridhiwa na Serikali ambazo ni: 1. Kufanya uchunguzi kwenye Makinikia yaliyopo Bandari ya Dar es Salaam, Bandari Kavu na migodini kwa kupekua na kubaini vitu vilivyomo ndani pamoja na kuchukua sampuli za makinikia ili kuzifanyia uchunguzi wa kimaabara.

2 of 13 2. Kufanya uchunguzi wa kimaabara na kubainisha aina, kiasi na viwango vya madini yatakayoonekana katika makinikia kisha kubainisha thamani ya madini hayo. 3. Kutumia mitambo ya scanners iliyopo katika Bandari ya Dar es Salaam kwa ajili ya kujiridhisha na aina ya shehena zilizomo kwenye makontena yenye mchanga wa madini; hii ni pamoja na kubainisha uwezo wa scanners hizo kuona vitu vyenye ukubwa na maumbile tofauti vilivyomo ndani ya makontena yenye makinikia. 4.

Kuchunguza utendaji wa Wakala wa Serikali wa Ukaguzi Madini (TMAA) wa kuchukua sampuli za makinikia, uchunguzi wa madini kwenye maabara na utaratibu wa ufungaji wa utepe wa udhibiti (seal) kwenye makontena kabla ya kusafirishwa nje ya nchi.5. Kamati pale itakapoona inafaa inaweza kuongeza Hadidu za Rejea katika kuboresha utekelezaji wa majukumu yake.

Aidha, Kamati itakuwa na mamlaka ya kumwita mtu yeyote kwa lengo la kupata taarifa. Utekelezaji wa Majukumu Ili kutekeleza uchunguzi huu, Kamati ilifanya yafuatayo: 1. Kuandaa mpango kazi. 2. Kukusanya nyaraka na taarifa mbalimbali kuhusiana na makontena yenye makinikia yaliyozuiliwa na Serikali kusafirishwa nje ya nchi. 3. Kutembelea maeneo yote yenye makontena yenye shehena za makinikia ili kuyachunguza na kuchukua sampuli zake.

Maeneo hayo ni Bandari 3 of 13 ya Dar es Salaam, Bandari Kavu – ZAM CARGO na migodi ya Bulyanhulu na Buzwagi. 4. Kutathmini uwezo wa scanners wa kuonesha makinikia yaliyomo ndani ya makontena pamoja na vitu vingine ambavyo vinaweza kuwa ndani ya makinikia.

5. Kufanya uchunguzi wa kimaabara wa sampuli za makinikia na kubaini aina, viwango na kiasi cha madini yaliyomo kwenye makinikia. 6. Kukokotoa thamani ya madini yaliyopimwa kwenye makinikia kwa kutumia viwango vilivyopatikana kutokana na uchunguzi wa kimaabara pamoja na thamani ya madini hayo kwenye soko la dunia.

7. Kuchunguza utendaji wa Wakala wa Serikali (TMAA) wa kukagua na kudhibiti uzalishaji na usafirishaji wa makinikia. Matokeo ya Uchunguzi Matokeo makuu ya uchunguzi huu ni yafuatayo: 1. Dhahabu Kamati imebaini kuwepo kwa viwango vingi vya juu vya dhahabu ndani ya makinikia yaliyofanyiwa uchunguzi.

Viwango hivyo ni kati ya 671 g/t hadi 2375 g/t, sawa na wastani wa 1400 g/t. Wastani huu ni sawa na 28 kg za dhababu kwenye kontena moja lenye tani 20 za makinikia. Hivyo, kwenye makontena 277 ya makinikia yaliyozuiliwa Bandari ya Dar es Salaam na Bandari Kavu yatakuwa na wastani wa tani 7.8 za dhahabu yenye thamani ya TZS bilioni 676 (USD 307,292,720).

Aidha, kwa kutumia kiwango cha juu kilichopimwa kwenye kontena moja lenye shehena ya tani 20 za makinikia (47.5 kg), kiasi cha dhahabu katika makontena 277 kitakuwa 13,157.5 kg ambazo thamani yake ni TZS 1,146,860,330,000 (USD 521,300,150). 4 of 13 Hivyo, thamani ya dhahabu katika makontena 277 yaliyozuiliwa bandarini ni kati ya TZS bilioni 676 na bilioni 1,147.

Taarifa tulizopata kutoka kwa wazalishaji pamoja na Wakala wa Serikali wa Ukaguzi Madini (TMAA) zinaonesha kuwa makinikia yana wastani wa takriban 200 g/t. Kiwango hiki ni sawa na kilo 4 za dhababu kwenye kila kontena. Hivyo, makontena 277 ya makinikia yaliyozuiliwa Bandari ya Dar es Salaam na Bandari Kavu yatakuwa na tani 1.1 za dhahabu. Kiasi hiki cha dhahabu kina thamami ya TZS bilioni 97.5 (USD 44,320,000).

Thamani hii ni ndogo sana ukilinganisha na thamani halisi iliyopatikana katika uchunguzi huu ya kati ya TZS bilioni 676 na bilioni 1,147. Kutokana na tofauti hii kubwa kati ya viwango vya dhahabu vilivyopo kwenye taarifa za usafirishaji na vile ambavyo Kamati imevibaini, ni dhahiri kuwa Taifa linaibiwa sana kupitia usafirishaji wa makinikia nje ya nchi. 2.

Pamoja na viwango vikubwa vya dhahabu kwenye makinikia, Kamati ilipima na kupata viwango vikubwa vya madini ya copper (kiwango cha 15.09% hadi 33.78%, wastani wa 26%), silver (kiwango cha 202.7 g/t hadi 351 g/t, wastani wa 305 g/t), sulfur (kiwango cha 16.7% hadi 50.8%, wastani wa 39.0%) na iron (kiwango cha 13.6% hadi 30.6%, wastani wa 27%).

Copper Wastani wa kiwango cha copper kilichopatikana ni tani 5.2 na kiwango cha juu kilichopimwa ni tani 6.75 kwenye kila kontena lenye tani 20 za makinikia. Hivyo, kiasi cha wastani wa copper kwenye makontena 277 ni tani 1,440.4 ambazo thamani yake ni TZS bilioni 17.9 (USD 8,138,260) na kiasi cha juu ni tani 1,871.4 ambazo zina 5 of 13 thamani ya TZS bilioni 23.3 (USD 10,573,478).

Hivyo, thamani ya copper katika makontena 277 yaliyozuiliwa bandarini ni kati ya TZS bilioni 17.9 na bilioni 23.3. Nyaraka za usafirishaji ambazo Kamati ilizipata kutoka bandarini zinaonesha kuwa makinikia yana wastani wa kiwango cha copper cha 20%. Kiwango hiki ni sawa na tani 4 za copper kwenye kila kontena; hivyo makontena 277 yaliyozuiliwa bandarini yatakuwa na tani 1,108 za copper. Kiasi hiki cha copper kina thamami ya USD 6,204,800 sawa na TZS bilioni 13.6.

Kwa takwimu hizi, kwa upande wa copper nako kuna upotevu mkubwa wa mapato ya taifa ukizingatia kuwa usafirishaji wa makinikia nje ya nchi umefanyika kwa muda mrefu. Silver Wastani wa kiwango cha silver kilichopimwa ni 6.1 kg na kiwango cha juu ni 7 kg kwa kontena lenye tani 20 za makinikia. Hivyo, kiasi cha wastani wa silver kwenye makontena 277 ni 1,689 kg (tani 1.7) ambazo thamani yake ni TZS bilioni 2.1 (USD 937,446); kiasi cha juu ni 1,939 kg (tani 1.9) ambazo thamani yake ni TZS bilioni 2.4 (USD 1,075,757).

 

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here