LSF wakutana na Wahariri wa vyombo vya Habari kwenye Warsha ya msaada wa Kisheria

0
143

Mfuko wa Fedha za Msaada wa Kisheria (LSF),umeenda warsha maalum kwa Wahariri wa vyombo vya Habari nchini juu ya mchango wa vyombo vya habari katika kusaidia taasisi zinazotoa msaada wa sheria kwa jamii katika maeneo mbalimbali ya Tanzania Bara na Visiwan.

Awali akitoa utambulisho namna mfuko huo unavyofanya shughuli zake pamoja na kufikia malengo yake mbalimbali, Mtendaji Mkuu wa LSF, Kees Groenendijk ameeleza kuwa, mfuko huo umeweza kufikia malengo mbalimbali ya utoaji msaada wa kisheria kwa Jamii hasa iliyo pembezoni  kwa kuwafikia na kutoa misaada y kisheria.

Kwa upande wake, mwezeshaji wa warsha hiyo, Mwanasheria Harold Sungusia aliweza kuwasilisha mada namna vyombo vya habari vinavyoweza kusaidia upatikanaji wa haki kwa ujumla kwa jamii ikiwemo kujua masuala yanayohusu kisheria  na namna ya nyenzo za kuzifuata kama Wanahabari na Vyombo vya habari.

Mwanasheria Harold Sungusia akionesha moja ya kitabu juu ya sheria  kwa baadhi ya wahariri na wanahabari waandamizi katika semina kwa wanahabari iliyoandaliwa na LSF. Wanatasnia hao wa habari wamepata fursa ya kujadiliana kwa pamoja na LSF namna vyombo vya habari vinavyoweza kusaidia upatikanaji wa haki kwa ujumla kwa jamii.

Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Fedha za Msaada wa Kisheria (LSF), Kees Groenendijk akiwasilisha mada kwa baadhi ya wahariri na wanahabari waandamizi katika semina kwa wanahabari iliyoandaliwa na LSF. Mfuko huo umeweza kukutana na baadhi ya wahariri na waandishi waandamizi na kutoa semina juu ya mchango wa vyombo vya habari katika kusaidia taasisi zinazotoa msaada wa sheria kwa jamii.

Baadhi ya wahariri na waandishi wa habari waandamizi kutoka vyombo mbalimbali vya habari wakiwa katika semina iliyoandaliwa na Mfuko wa Fedha za Msaada wa Kisheria (LSF) kwa na kuzungumzia mchango wa vyombo vya habari katika kusaidia taasisi zinazotoa msaada wa sheria kwa jamii

Meneja Mawasiliano wa Mfuko wa LSF, Robert Zephania akizungumza katika semina hiyo. 

Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Fedha za Msaada wa Kisheria (LSF), Kees Groenendijk akizungumza na waandishi wa habari wakati wa tukio hilo.

Mfuko huo umeweza kukutana na baadhi ya wahariri na waandishi waandamizi na kutoa semina juu ya mchango wa vyombo vya habari katika kusaidia taasisi zinazotoa msaada wa sheria kwa jamii.

Baadhi ya washiriki wa semina hiyo wakiwa katika picha ya pamoja 

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here