KISA: Mfanyakazi na Mwajili wake katika kuamini kwamba riziki inatoka kwa Allah

0
292

Kulikua na mtu mmoja anamlea mama yake na mkewe, na alikua anafanya kazi ya utumishi kwa bosi mmoja, na alikua anatimiza majukumu ya kazi yake vizuri.

Siku moja hakuweza kufika kazini, bosi wake akasema katika nafsi yake lazima nimuongezee mshahara hata isitokee siku kutofika kazini, na kwa hakika hatoacha kuja kwa matumaini ya kuongezewa mshahara,

Pindi alipokuja siku ya pili yake akampa mshahara wake na akamuongezea kama alivyoahidi, lakini yule mfanyakazi hakuzungumza chochote na wala hakumuuliza bosi wake…sababu ya kumuongezea mshahara.

Na baada ya muda yule mtumishi hakutokea kazini kwa mara nyengine, bosi akakasirika sana na akasema;” nitampunguzia mshahara niliomuongezea,alipokuja kazini akampunguzia mshahara.
lakini yule mfanyakazi hakusema chochote na wala hakumuuliza bosi wake.. sababu ya kumpunguzia mshahara.

Bosi wake akashangazwa sana kwa kitendo kile,kisha akasema kumwambia: “Nilikuongezea mshahara hukusema chochote ,na nimekupunguzia hukusema chochote.”- Yule mfanyakazi akasema: “Siku ya kwanza ambayo sikutokea kazini mwenyezi mungu alijaalia mtoto, na kwa ajili hio ndio maana sikutokea kazini, basi uliponiongezea mshahara nikasema hii ni riziki ya mtoto wangu amekuja nayo.

Na niliposhindwa kuja mara ya pili Mama yangu alikua amefariki, na wakati uliponipunguzia mshahara nikasema hii ni riziki yake ameondoka nayo.

Uzuri ulioje kwa mtu kutosheka na kuridhia kile ambacho mwenyezi mungu amempa, na kuamini kwamba riziki inatoka kwa Allah.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here