Mbunge wa Chalinze Ridhiwani Kikwete aunga mkono juhudi za Clouds Media harambee ya MOYO 100

0
249

Mbunge wa Chalinze,Mkoani Pwani Mh. Ridhiwani Kikwete jana Mei 26.2017, amekuwa miongoni mwa watanzania waliojitokeza katika kuchangia kampeni maalum ya kusaidia fedha za matibabu ya upasuaji wa ugonjwa wa Moyo kwa watoto 100,kampeni iliyoanzishwa na Clouds Media Group.

Katika kampeni hiyo yenye lengo la kuchangia Sh. Milioni 200, ili kuweza kutibiwa watoto 100, katika Hospitali ya Moyo ya Jakaya Kikwete iliyopo Muhimbili Jijini Dar es Salaam, wati mbalimbali walifika katika kituo hicho cha Clouds na kuhamasisha uchangiaji wa fedha, huku Mbunge huyo wa Chalinze, Ridhiwani kupitia yeye na wadau wake waliweza kuchangia Sh milioni 10.

“Hongereni sana @cloudsfmtz na @cloudstv na hospitali ya Moyo ya Taasisi ya Jakaya Kikwete kwa kuanzisha jitihada hizi za kusaidia Tanzania. Imani yangu ukisaidia Mtoto umesaidia Taifa na umelivusha Taifa. Watoto ndiyo Tanzania yetu.

Katika kuunga mkono juhudi hizo , Mimi Ridhiwani Kikwete, Familia yangu, wadogo zangu, Mizega Foundation na Marafiki zangu tumechangia fedha shilingi Milioni Kumi ( Tshs. 10M). Imani yangu nimejitahidi kuchangisha . Wito ni Wananchi wenzangu wenye kiasi hata shilingi laki mbili wachangie watoto hawa .” alieleza Mbunge huyo Ridhiwani.

BONGONEWS unawatakiwa kila lakheri watoto hao zaidi ya 100, ambao wataenda kufanyiwa upasuaji wao ilikurudisha tabasamu lao. Tunaungana na Clouds katika jambo ili jema.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here