Rais Dkt. Magufuli amuapisha rasmi Inspekta Jenerali wa Polisi (IGP) Simon Sirro Ikulu Dar

0
199

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli leo tarehe 29 Mei, 2017 amemuapisha Kamishna wa Polisi Simon Nyakoro Sirro kuwa Mkuu wa Jeshi la Polisi (IGP).

Hafla ya kuapishwa kwa IGP Simon Nyakoro Sirro imehudhuriwa na Makamu wa Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan, Kaimu Jaji Mkuu wa Tanzania Mhe. Prof. Ibrahim Hamis Juma, Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Mhe. Mwigulu Lameck Nchemba, Naibu Mwanasheria Mkuu wa Serikali Mhe. Gerson John Mdemu, Viongozi wa vyombo vya ulinzi na usalama, Makatibu Wakuu wa Wizara na viongozi wa Mkoa wa Dar es Salaam wakiongozwa na Mkuu wa Mkoa huo Bw. Paul Christian Makonda.

Kabla ya IGP Simon Nyakoro Sirro kuapishwa kuwa Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini, Mhe. Rais Magufuli amemvua cheo cha zamani cha Kamishna wa Polisi na kumvalisha cheo kipya cha Inspekta Jenerali wa Polisi.

Katika hafla hiyo IGP Simon Nyakoro Sirro, pia amekula kiapo cha uadilifu kwa viongozi wa umma kilichoongozwa na Katibu wa Utumishi wa Umma kutoka Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma Bw. John Marko Kaole.

IGP Simon Nyakoro Sirro amechukua nafasi ya Ernest Mangu ambaye atapangiwa kazi nyingine.

Gerson Msigwa, Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, IKULU

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimvalisha vyeo vipya Inspekta Jenerali wa Polisi(IGP) Simon Sirro kabla ya kumuapisha Ikulu jijini Dar es Salaam

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimvalisha vyeo vipya Inspekta Jenerali wa Polisi(IGP) Simon Sirro kabla ya kumuapisha Ikulu jijini Dar es Salaam

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimuapisha Inspekta Jenerali wa Polisi(IGP) Simon Sirro Ikulu jijini Dar es Salaam.

Inspekta Jenerali wa Polisi(IGP) Simon Sirro akila kiapo Ikulu jijini Dar es Salaam.

Inspekta Jenerali wa Polisi(IGP) Simon Sirro akila kiapo cha uadilifu Ikulu jijini Dar es Salaam.

Inspekta Jenerali wa Polisi(IGP) Simon Sirro akisaini Hati ya Kiapo cha Uadilifu Ikulu jijini Dar es Salaam.

Inspekta Jenerali wa Polisi(IGP) Simon Sirro mara baada ya kula kiapo Ikulu jijini Dar es Salaam.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika picha ya pamoja na Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan, Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi, Kaimu Jaji Mkuu wa Tanzania Profesa Ibrahim Juma, Waziri wa Mambo ya Ndani ya nchi Mwigulu Nchemba,IGP mpya Simon Sirro,  IGP wa zamani Ernest Mangu pamoja na viongozi mbalimbali wa Jeshi la Polisi pamoja na Magereza.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika picha na Inspekta Jenerali wa Polisi(IGP) Simon Sirro pamoja na IGP wa zamani Ernest Mangu Ikulu jijini Dar es Salaam.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na IGP wa zamani Ernest Mangu Ikulu jijini Dar es Salaam

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na viongozi mbalimbali wa Majeshi ya Polisi na Jeshi la Wananchi  mara baada ya kumuapisha IGP Simon Sirro Ikulu jijini Dar es Salaam.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na viongozi mbalimbali wa Majeshi ya Polisi na Jeshi la Wananchi  mara baada ya kumuapisha IGP Simon Sirro Ikulu jijini Dar es Salaam.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Mwigulu Nchemba mara baada ya tukio la uapisho wa IGP Ikulu jijini Dar es Salaam. PICHA NA IKULU

 

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here