Britam Insurance Tanzania wazindua BIMA ya Afya kwa Makampuni, Ni maalum kwa wagonjwa wa kulazwa

0
171

*Wateja kunufaika huduma za matibabu katika Hospitali kubwa katika nchi 7,ikiwemo Afrika Kusini na Apolo India

Kampuni ya  Bima ya Britam Insurance Tanzania, Imezindua rasmi huduma mpya kwa wagonjwa wanaolazwa ambayo ni maalum kwa Wafanyakazi wa makampuni Makubwa, ya Kati na Madogo yaliyopo hapa nchini ambapo wateja wao watapata huduma bora katika Hospitali zaidi ya 10 kubwa zilizopo hapa nchini pamoja na Mataifa mengine ikiwemo India katika Hospitali ya Apollo na Hospitali za Afrika Kusini.

Akizungumza na waandishi wa Afisa Mtendaji Mkuu wa Britam Insurance Tanzania, Stephen Lokonyo amebainisha kuwa, wao wameangalia mahitaji halisi ya wateja wao wanataka nini hivyo wamekuja na ubunifu huo katika masuala ya BIMA kwa wananchi wote kupitia Makampuni yao.

“Lengo letu ni kuunga mkono na jitihada za Sera za Tanzania za kuhakikisha BIMA zinafika mbali hasa kwa wananchi wake wote. Tunatambua mtu ama mfanyakazi anapokuwa amelazwa, anatumia gharama kubwa sana za matibabu na pia shughuli za kiuchumi zinasimama. Kwa kuzingatia Huduma hii mpya wateja wetu watanufaika na gharama zetu ni za kiwango cha kawaida na tunakaribisha makampuni yote” alieleza Lokonyo.

Kwa upande wake,  Meneja wa Bima ya Afya wa Britam Insurance Tanzania, Christine Mwangi amebainisha kuwa, miongoni mwa faida ambazo wateja wao hao wa Makampuni watakazozipata katika kugharamia bima hizo za kulazwa ni zile ambazo zitahusu matibabu ya kulazwa hasa katika magonjwa mbalimbali yakiweo yale makubwa ambayo yatamfanya kulazwa.

“Huduma hii ya Afya kwa Makampuni ni maalum kwa ajili ya wagonjwa wa kulazwa pekee. Kampuni yetu ya Britam imeingia mikataba zaidi ya Hospitali kubwa 10 kwa Tanzania, Ikiwemo Hospitali ya Taifa Muhimbili, Hindu Mandali, Tumaini Hospital, Kairuki  Hospital, TMJ,HBG na zingine nyingi.

Pia wateja wetu watapata huduma hii katika Hospitali za nje ya Tanzania ikiwemo Nairobi Kenya, Afrika ya Kusini pamoja na Hospitali kubwa ya Napollo ya nchini India” alieleza  Meneja huyo wa Bima wa Britam, Bi. Christine Mwangi.

Naye Meneja wa Mauzo wa Britam Insurance Tanzania, Godfrey Mzee ameeleza kuwa, kampuni hiyo  imekuwa ikifanya shughuli zake za BIMA kwa miaka mingi, huku ikiweza kuwa katika matawi zaidi ya Saba katika nchi mbalimbali za Afrika Mashariki na Afrika kwa ujumla na ikijiendesha kwa kiwango kikubwa.

“Hadi sasa tayari makampuni mbalimbali yameanza kujitokeza na tupo nao katika hatua za mwisho kwenye makubaliano  ya huduma hii mpya ya Bima ya kulazwa. Milango ipo wazi kwa makampuni yote” alieleza Godfrey Mzee.

Bima hiyo mpya inalenga kwa wagonjwa wa kulazwa pekee ambapo kupitia makampuni yatakayojiunga wateja wake watapata fursa za matibabu ikiwemo ugonjwa Kansa, Matatizo ya figo, Athima na magonjwa mengine mengi.

Tazama hapa kuona tukio hilo:

Baadhi ya Wageni waalikwa, Wadau na Wafanyakazi wa Kampuni ya  Bima ya Britam Insurance Tanzania,  wakiadilishana mawazo wakati wa uzinduzi wa huduma mpya kwa wagonjwa wanaolazwa wakati wa uzinduzi huo uliofanyika Jijini Dar es Salaam, jana Mei 30.2017.

Baadhi ya Wageni waalikwa, Wadau na Wafanyakazi wa Kampuni ya  Bima ya Britam Insurance Tanzania,  wakiadilishana mawazo wakati wa uzinduzi wa huduma mpya kwa wagonjwa wanaolazwa wakati wa uzinduzi huo uliofanyika Jijini Dar es Salaam, jana Mei 30.2017.

Mgeni rasmi akipokelewa na wajumbe wa kampuni hiyo ya Britam wakati wa kuwasili kwenye tukio hilo la uzinduzi

Mgeni rasmi akiwa na ajumbe wa kampuni hiyo ya Britam wakati wa kuwasili kwenye tukio hilo la uzinduzi

‘MC’ wa shughuli hiyo, Taji Lihundi akiongoza shughuli hiyo

Baadhi ya Wageni waalikwa, Wadau na Wafanyakazi wa Kampuni ya  Bima ya Britam Insurance Tanzania,  wakiadilishana mawazo wakati wa uzinduzi wa huduma mpya kwa wagonjwa wanaolazwa wakati wa uzinduzi huo uliofanyika Jijini Dar es Salaam, jana Mei 30.2017.

Mjumbe katika kampuni ya Britam Insurance Tanzania, Mike Laiser akimkaribisha mgeni rasmi kuzindua huduma hiyo

Mgeni rasmi katika tukio hilo Mkurugenzi wa shughuli za Bima-Shirika la Bima Tanzania (TILA), Samwel Mwiru  akizungumza wakati wa tukio hilo

Mgeni rasmi katika tukio hilo Mkurugenzi wa shughuli za Bima-Shirika la Bima Tanzania (TILA), Samwel Mwiru  akivuta kitambaa wakati wa zoezi la kuzindua rasmi huduma hiyo

Mgeni rasmi katika tukio hilo Mkurugenzi wa shughuli za Bima-Shirika la Bima Tanzania (TILA), Samwel Mwiru  akiwa pamoja na viongozi wa Britam Insurance Tanzania wakati wa zoezi la kuzindua rasmi huduma hiyo

Mgeni rasmi katika tukio hilo Mkurugenzi wa shughuli za Bima-Shirika la Bima Tanzania (TILA), Samwel Mwiru  akiwa pamoja na wafanyakazi wa Britam Insurance Tanzania wakati wa zoezi la kuzindua rasmi huduma hiyo

Mgeni rasmi katika tukio hilo Mkurugenzi wa shughuli za Bima-Shirika la Bima Tanzania (TILA), Samwel Mwiru  akiwa akiwa katika tukio hilo 

Mgeni rasmi katika tukio hilo Mkurugenzi wa shughuli za Bima-Shirika la Bima Tanzania (TILA), Samwel Mwiru  akizungumza na waandishi wa Habar mara baada ya kuzindua rasmi  huduma hiyo

Mtendaji Mkuu wa Britam Insurance Tanzania, Stephen Lokonyo akizungumza na waandishi wa Habari wakati wa tukio hilo

Mjumbe katika kampuni ya Britam Insurance Tanzania, Mike Laiser akizungumza katika tukio hilo.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here