Kikosi cha Taifa Stars wapiga mazoezi ya ‘Jaza Ujazwe’ Misri

0
218

Wachezaji wa timu ya Tanzania ya Mpira wa Miguu ‘Taifa Stars’   waliopo nchini Misri katika kambi maalum wapo katika mazoezi makali na ya aina yake ambayo tunaweza kuyaita ‘Jaza Ujazwe’kwani Kocha Mkuu wa Stars, Salum Mayanga ameamua kuwapigisha zoezi la usiku  pamoja na lile la asubuhi.

Kwa tizi hilo la usiku na asubuhi kama alivyobainisha Kocha toka walipotua nchini humo  linaendana na msemo unaokua kwa kasi sana hapa nchini Tanzania wa ‘Jaza Ujazwe’ ambao ni kauli mbiu ya moja ya kampuni ya simu kuhamasisha wateja wao kuweka kiasi na kuongezewa MB za kuperuzi zaidi mitandaoni vivyohivyo kwa Stars sasa wanapiga tizi kali ili kuja kupata ushindi mnono ili kuweza kujiweka mazingira safi ya kuwania tiketi ya kucheza fainali za Kombe la Mataiafa ya Afrika (AFCON) za mwaka 2019 zitakazofanyika Cameroon.

Kikosi hicho kimeweka kambi katika Hoteli ya Tolip Sports City, Alexandria nchini Misri l na Juni mosi, mwaka huu. Taifa Stars inayodhaminiwa Bia ya Serengeti kutoka Kampuni ya Bia ya SBL, inajiandaa kushindana na Lesotho Juni 10, 2017 kwenye uwanja wa Taifa Jijini Dar es Salaam.

Kibuyu katika mpira wa miguu hatari, hapo Erasto Nyoni (katikati), akiwania mpira wa Hassan Kessy (kulia) baada ya miguu yao kukutana kupiga mpira ‘kibuyu’ uliopaa juu huku wenzao wakiwashuhudia kwenye mazoezi leo asubuhi. Taifa Stars inayodhaminiwa Bia ya Serengeti kutoka Kampuni ya Bia ya SBL, inajiandaa kushindana na Lesotho Juni 10, 2017 kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam kuwania tiketi ya kucheza fainali za Kombe la Mataiafa ya Afrika (AFCON) za mwaka 2019 zitakazofanyika Cameroon.

Makipa wa Taifa Stars kutoka kushoto, Aishi Manula na Benno Kakolanya wakivuta pumzi baada ya mazoezi ya timu ya Tanzania ya Mpira wa Miguu ‘Taifa Stars’ yaliyofanyika jana usiku kwenye Uwanja wa Tolip Sports City jijini Alexandria jana usiku Mei 31, 2017. Taifa Stars inayodhaminiwa Bia ya Serengeti kutoka Kampuni ya Bia ya SBL, inajiandaa kushindana na Lesotho Juni 10, 2017 kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam kuwania tiketi ya kucheza fainali za Kombe la Mataiafa ya Afrika (AFCON) za mwaka 2019 zitakazofanyika Cameroon.

Wachezaji wa Stars wakinyoosha miili baada ya mazoezi ya nguvu yaliyofanyika leo. Taifa Stars inayodhaminiwa Bia ya Serengeti kutoka Kampuni ya Bia ya SBL, inajiandaa kushindana na Lesotho Juni 10, 2017 kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam kuwania tiketi ya kucheza fainali za Kombe la Mataiafa ya Afrika (AFCON) za mwaka 2019 zitakazofanyika Cameroon.

Wachezaji wa Stars wakiwania mpira katika mazoezi ya nguvu yaliyofanyika leo. Taifa Stars inayodhaminiwa Bia ya Serengeti kutoka Kampuni ya Bia ya SBL, inajiandaa kushindana na Lesotho Juni 10, 2017 kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam kuwania tiketi ya kucheza fainali za Kombe la Mataiafa ya Afrika (AFCON) za mwaka 2019 zitakazofanyika Cameroon.

Kocha Mkuu wa Taifa Stars, Salum Mayanga (kushoto) na Meneja wa timu hiyo, Danny Msangi wakiwashuhudia wachezaji wa Stars wakipooza miili yao kwenye bwawa la kuogelea katika Hoteli ya Tolip Sports City, Alexandria nchini Misri leo asubuhi Juni mosi, mwaka huu. Taifa Stars inayodhaminiwa Bia ya Serengeti kutoka Kampuni ya Bia ya SBL, inajiandaa kushindana na Lesotho Juni 10, 2017 kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam kuwania tiketi ya kucheza fainali za Kombe la Mataiafa ya Afrika (AFCON) za mwaka 2019 zitakazofanyika Cameroon.

Makipa wa Taifa Stars kutoka kushoto, Said Mohammed, Aishi Manula na Benno Kakolanya wakivuta pumzi baada ya mazoezi ya timu ya Tanzania ya Mpira wa Miguu ‘Taifa Stars’ yaliyofanyika jana usiku kwenye Uwanja wa Tolip Sports City jijini Alexandria jana usiku Mei 31, 2017. Taifa Stars inayodhaminiwa Bia ya Serengeti kutoka Kampuni ya Bia ya SBL, inajiandaa kushindana na Lesotho Juni 10, 2017 kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam kuwania tiketi ya kucheza fainali za Kombe la Mataiafa ya Afrika (AFCON) za mwaka 2019 zitakazofanyika Cameroon.

IMETOLEWA NA SHIRIKISHO LA MPIRA WA MIGUU TANZANIA

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here