Ofa ya kutembelea bure Siku 3 hifadhi za Taifa, Watanzania 6,368 wajitokeza

0
188

Baada ya Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira kwa kushirikiana na Wizara ya Mali Asili na Utalii kupitia Shirika la Hifadhi za Taifa (TANAPA) kuruhusu watanzania kuingia kwenye hifadhi za wanyamapori nchini bila kulipia kiingilio, watanzania takribani 6,368 walitembelea hifadhi hizo kuanzia Juni 2 -4, 2017.

Kwa mujibu wa taarifa kwa vyombo vya habari iliyotolewa na Meneja Mawasiliano TANAPA, Pascal Shelutee inaonhyesha hifadhi ya Ziwa Manyara iliongoza kwa kupokea wageni 1,582 ikifuatiwa na Serengeti iliyopokea wageni 1,085 na Mikumi iliyotembelewa na watu 1004.

Pia imeataja hifadhi zilipokea wageni wachache kuwa ni Kitulo mkoani Mbeya iliyotembelewa na wageni 13 na Mkomanzi mkoani Kilimanjaro na Tanga iliyotembelewa na wageni 43.

“TANAPA itaendelea kuelimisha watanzania juu ya umuhimu wa kutembelea vivutio vya utalii katika hifadhi za Taifa, shirika litaendelea kushirikiana na wadau kuboresha miundombinu nje ya hifadhi hususan barabara zinazopitika wakati wote ili kuvuta wananchi wengi kutembelea hifadhi,” inaeleza sehemu ya taarifa hiyo.

Ofa ya siku mbili kwa watanzania kutembelea hifadhi za wanyamapori, ilitolewa ili kuadhimisha siku ya Mazingira duniani.

Hifadhi ya Kitulo

Mkomanzi

Hifadhi ya Ziwa Manyara

Hifadhi ya Serengeti

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here