Waziri Ummy azindua rasmi huduma ya upasuaji na upandikizaji kifaa cha usikivu kwa Watoto Muhimbili

0
329

Waziri Ummy azindua rasmi huduma ya upasuaji na upandikizaji kifaa cha usikivu kwa Watoto Muhimbili

Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mh. Ummy Mwalimu amezindua rasmi Huduma ya Upasuaji na Upandikizaji kifaa cha usikivu kwa Watoto waliozaliwa na tatizo hilo, tukio lililofanyika mapema leo  Juni 7.2017 katika Hospitali ya Taifa Muhimbili.

Waziri Ummy katika kuzindua huduma hiyo, amebainisha kuwa kuanzia sasa Serikali haitagharamia matibabu ya huduma hiyo nje ya nchi, ila kwa atakayetaka kwenda nje ataenda kwa gharama zake mwenyewe.

“Nazindua rasmi huduma hii ya kuwekewa vifaa vya usikivu (Cochlear Implant). Huduma hii sasa inapatikana Muhimbili hivyo basi kuanzia leo Serikali haitagharamia matibabu ya mgonjwa  nje ya nchi kwa ajili ya kupandikizwa kifaa hichi cha usikivu. Kama mtu atataka kwenda nje, ataenda kwa gharama zake mwenyewe ila kama atafadhiliwa na serikali, atafanyiwa hapa hapa nchini” amesema Waziri Ummy Mwalimu wakati wa  tukio hilo la uzinduzi.

Aidha,Waziri Ummy amebainisha kuwa baada ya kufanikiwa katika hatua hiyo ya upandikizaji vifaa vya usikivu, Mwezi  Julai wanatarajia kuzindua  huduma nyingine ya upandikizaji figo hii ni katika kufikia malengo ya Nchi kuwasogezea huduma muhimu na kubwa ambazo zilikuwa zikigharimu mabilioni ya pesa kwa wagonjwa kwenda kutibiwa nje ya nchi.

“Sisi tupo tayari katika utoaji wa huduma bora. Huduma hii sasa inapatina hapanchini kwa hiyo katika utoaji wa huduma ya kibobezi na kibingwa ni eneo ambalo tumepiga hatua sana Serikali ya awamu ya tano. Na ninafurahi sana mwezi wa ujao wa saba tunakuja tena na huduma nyngine ya kupandikiza figo.

Kwa kuwa ugnjwa wa saratani ndio unaongoza kwa asilimia 50 hadi 60 kupeleka wagonjwa nje, tumeagiza kifaa maalum cha kutoa matibabu ya saratani ambacho pia hakipo katika nchi yoyote ile za Afrika Mashariki hivyo tutapiga hatua kubwa sana” alimalizia Waziri Ummy Mwalimu.

Kwa upande wake, Mkurugenzi wa Hospitali ya Taifa Muhimbili, Profesa Lawrence Museru alimshukuru Waziri Ummy Mwalimu ambapo pia alibainisha kuwa, tatizo hilo la usikivu limekuwa likiongezeka katika jamii ya watanzania kama ilivyo kote Duniani. Hata hivyo amebainisha kuwa utafiti wa makadirio ya Hospitali unaonyesha kuwa kwa mwaka takribani watoto kati 200 watahitaji huduma hiyo hapa nchini kwa mwaka.

“Utaalamu ambao umeendelezwa takribani miaka 20 ya hivi karibuni unaonyesha kuwa watoto hawa wakigundulika mapema na kuwekewa vifaa vya usikivu (Cochlear Implant) wataishi kama kawaida, wakati wasipopata huduma hii watakuwa viziwi” amesema Prof. Museru.

Hata hivyo kwa hapa nchini kwa mara ya kwanza  mwaka 2003,Muhimbili ilipeleka mgonjwa mmoja kwenda kutibiwa nchini India tangu hapo wagonjwa wanaohitaji huduma hiyo wamekuwa wakiongezeka huku huduma hiyo ikiwa na gharama kubwa inayofikia hadi kati ya Tsh. Milioni 80 hadi Mil 100 kwa mgonjwa mmoja. Hata hivyo hadi  mwaka jana ni wgonjwa 50 tu waliokuwa wamefaidka  kupata huduma hiyo ya ufadhili kutoka Serikalini.

Kuanzishwa  kwa huduma hii hapa nchini, Serikali itapunguza gharama kwa asilimia 60 na kufikia wastani wa  Tsh. Milioni 36 kwa mgonjwa mmoja kutoka wastani wa Milioni 100 huku zikiwa milioni 250 hadi Milioni 300 zikiokolewa kwa kufanya upasuaji huu hapa nchini na hii inaweza kutoa huduma ya wagonjwa wengi zaidi.

Prof. Museru amebainisha kuwa,  kwa mwaka huu 2017, wanatarajia kufanyia wagonjwa 24, namba ambayo itaongezeka baada ya kusomesha wataalam wengi zaidi nje ya nchi.

Aidha, Prof. Museru alimshukuru Mohamed El Disouky na wenzake kutoka kampuni ya Medel ambayo imekuwa pamoja na Muhimbili kwa muda mrefu ikisaidiana katika utayarishaji wataalamu na miundombinu ya kuendeshea huduma hiyo.

Pia aliipongeza kampuni ya Hearwell inayoongozwa na Fayaz Jaffer wa Hearwell Clinic kwa kufanya kazi kwa ushirikiano mkubwa.

Wadau mbalimbali pamoja wanahabari wakiangalia namna zoezi la upandikizi wa vifaa vya usikivu kwa njia ya video wakati wa tukio hilo mapema leo Juni 7.2017, Muhimbili

Baadhi ya Wazazi wakiwa na watoto wao ambao tayari wamewekewa vifaa hivyo ya Usikivu

Waziri Ummy Mwalimu akifuatilia zoezi hilo wakati wa kuangalia video namna vifaa hivyo vya usikivu vinavyowekwa  kwa watoto

Waziri Ummy Mwalimu akizungumza katika tukio hilo

Ofisa Udhibiti Ubora wa NHIF, Dk. Raphael Mallaba akipkea maagizo kutoka kwa Waziri Ummy Mwalimu (hayupo pichani) wakati wa tukio hilo ambapo Waziri Ummy aliagiz NHIF kushughulikia mpango wa kuwa na huduma hiyo ya vifaa vya usikivu katika huduma zake za bima. 

Fayaz Jaffer wa Hearwell Clinic  akifuatiwa na Hassan Wahba akifuatiwa na Mohamed El Disouky wa Medel wakiangalia video hiyo inayoonesha namna ya upandikizaji wa vifaa vya usikivu kwa watoto

Fayaz Jaffer wa Hearwell Clinic akifafanua jambo kwa Waziri Ummy Mwalimu (Hayupo pichani) wakati wa tukio hilo la uzinduzi

Picha ya chini na juu: Waziri Ummy akipata picha  ya pamoja na baadhi ya watoto waliokwisha pandikizwa vifaa vya usikivu pamoja na wadau katika utoaji wa huduma hoyo na viongozi wa Hospitali ya Muhimbili wakipata picha ya pamoja.

Waziri Ummy Mwalimuu akimjulia hali mtoto wa kwanza kabisa aliyepata huduma hiyo ya kupandikizwa vifaa vya usikivu hapa nchini. aliyebebwa na mama yake wakati walipowatembelea wodini

Waziri Ummy akimjula hali mmoja wa watoto waliopta huduma hiyo

Waziri Ummy akipata maelezo kutoka kwa Mohamed El Disouky wa MEDEL ambao wamekuwa mchango mkubwa katika kusaidia huma hiyo hospitalini hapo

Waziri Ummy akisikiliza maelezo kutoka kwa Mohamed El Disouky wa MEDEL ambao wamekuwa mchango mkubwa katika kusaidia huma hiyo hospitalini hapo

Waziri Ummy akifurahia jambo kutoka kwa mmoja wa watoto ambao walishawekewa vifaa vya usikivu wakati wa tukio hilo la  uzinduzi wa huduma hiyo hapa nchini katika hospitalini ya Muhimbili.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here