ZANTEL YATOA MSAADA WA SARUJI NA MABATI KWA WAATHIRIKA WA MAFURIKO WA MKOA WA KUSINI PEMBA

0
115

Mkuu wa Kampuni ya mawasiliano ya Zantel-Zanzibar, Bw. Mohamed Khatib Baucha  amekabidhi vitu mbalimbali vya ujenzi  ikiwemo mfuko ya saruji na  Mabati  vifaa vilivyopokelewa na Mkuu wa Mkoa wa Kusini Pemba Mhe. Mwanajuma Majid Abdallah.

Msaada huo ni kwa ajili ya waathirika wa mafuriko yaliyotokea hivi karibuni katika mkoa huo. Zoezi la makabidhiano ya msaada huo lilifanyika jana mkoani humo ambapo Zantel walitoa jumla ya mabati 350 na Saruji mifuko 350, vyote vikigharimu Sh. 13 milioni.

Mkuu wa Mkoa wa Kusini Pemba Mhe. Mwanajuma Majid Abdallah akizungumza na wakuu wa wilaya za mkoa huo Mhe. Salama Mbarouk Khatib wa wilaya ya ChakeChake (kushoto) na Hemed Suleiman Abdallah wa wilaya ya Mkoani( wa pili kushoto) kabla ya kuwakabidhi msaada wa Saruji na Mabati yaliyotolewa na Kampuni ya Mawasiliano ya Zantel kwa ajili ya waathirika wa mafuriko yaliyotokea hivi karibuni katika mkoa huo. Zoezi hilo lilifanyika jana kisiwani Pemba-Zanzibar ambapo jumla ya mabati 350 na Saruji mifuko 350 yalikabidhiwa na Kampuni ya Zantel.

Mkuu wa Kampuni ya mawasiliano ya Zantel-Zanzibar, Bw. Mohamed Khamis Baucha (kushoto) akimkabidhi Mkuu wa Mkoa wa Kusini Pemba Mhe. Mwanajuma Majid Abdallah mifuko ya Saruji kwa kwa ajili ya waathirika wa mafuriko yaliyotokea hivi karibuni katika mkoa huo. Zoezi la makabidhiano ya msaada huo lilifanyika jana mkoani humo ambapo Zantel walitoa jumla ya mabati 350 na Saruji mifuko 350, vyote vikigharimu Sh. 13 milioni. Kushoto ni Ofisa wa fedha na Utawala wa Tawi la Zantel–Pemba, Yakoub Fadhil Juma

Mkuu wa Kampuni ya mawasiliano ya Zantel-Zanzibar, Bw. Mohamed Khamis Baucha (kushoto) akimkabidhi Mkuu wa Mkoa wa Kusini Pemba Mhe. Mwanajuma Majid Abdallah mabati kwa kwa ajili ya waathirika wa mafuriko yaliyotokea hivi karibuni katika mkoa huo. Zoezi la makabidhiano ya msaada huo lilifanyika jana kisiwani Pemba-Zanzibar ambapo Zantel walitoa jumla ya mabati 350 na Saruji mifuko 350, vyote vikigharimu Sh. 13 milioni.

Mkuu wa Mkoa wa Kusini Pemba Mhe. Mwanajuma Majid Abdallah akizungumza na wakuu wa wilaya za mkoa huo Mhe. Salama Mbarouk Khatib wa wilaya ya ChakeChake (kushoto) na Hemed Suleiman Abdallah wa wilaya ya Mkoani( wa pili kushoto) kabla ya kuwakabidhi msaada wa Saruji na Mabati yaliyotolewa na Kampuni ya Mawasiliano ya Zantel kwa ajili ya waathirika wa mafuriko yaliyotokea hivi karibuni katika mkoa huo. Zoezi hilo lilifanyika jana kisiwani Pemba-Zanzibar ambapo jumla ya mabati 350 na Saruji mifuko 350 yalikabidhiwa na Kampuni ya Zantel.

Mkuu wa Mkoa wa Kusini Pemba Mhe. Mwanajuma Majid Abdallah akiwakabidhi wakuu wa wilaya wa mkoa huo mabati yalitolewa na Kampuni ya Mawasiliano ya Zantel kwa ajili ya waathirika wa mafuriko yaliyotokea hivi karibuni katika mkoa huo.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here