ORIFLAME yasherehekea miaka 50 ya uuzaji wa bidhaa zake za vipodozi, yakutana na wadau wake Dar

0
211

Kampuni ya  Oriflame Tanzania inayouza vipodozi asilia mapema jana Juni 8.2017 imeweza kukutana na wadau wake mbalimbali kama familia ikiwemo wafanyabiashara, Wanahabari , Wafanyabiashara na watu maarufu wakiwemo  Wasanii na viongozi ambapo na kujumuka katika maadhimisho ya miaka 50 tokea kuanzishwa kwake, miaka 50 iliyopita huko nchini Sweden.

Tukio hilo limefanyika Jijini Dar e Salaam huku mgeni rasmi alikuwa Balozi wa Sweden Nchini Bi. Katarina Rangnitt alipongeza watanzania kuzipokea bidhaa za Oriflame  kwani zimeweza kuwasaidia na  kuwa bora kwani zimetengenezwa kwa ustadi mkubwa  ikiwemo kutumia vitu vya asili hasa mimea na matunda .

“Tunafurahia sana kuona bidhaa kutoka Sweden imeweza kuwa bora zaidi hapa Tanzania na Afrika. Imekuwa bidhaa hizi za Oriflame zimekuwa zikipendwa Duniani kote na hadi sasa tunaposheherekea miaka 50 ya kuanzishwa kwake” alieleza Balozi huyo wa Sweden, Bi. Katarina Ranginitt.

Kwa upande wake Mkuu wa  Masoko wa Oriflame Tanzania, Bi. Mary Riungu ameeleza kuwa, wana bidhaa mbalimbali ambapo zinapatikana pia kwa mawakala wao wote sehemu tofauti za mikoa ya Tanzania  ikiwemo majiji yote na mikoa hivyo amewahimiza wananchi kuchangamkia ofa ya bidhaa hizo kwani Oriflame ni moja ya makampuni makubwa Duniani.

“Bidhaa zetu ni bora na zinapendwa duniani kote ambapo katika ukubwa ni ya nne kidunia. Tunabidhaa mbalimbali zenye mahitaji kwa watu wote na kwa bei ambayo ni rafiki kabisa” alieleza Bi. Mary RiungU.

Nae Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Oriflame kwa Nchi za Afrika, Piyush Chandra amebainisha kuwa, wamekuwa na  bidhaa mpya  na za tofautitofauti  kwenye soko la Afrika Mashariki ikiwemo vipodozi maalum vitakavyokufanya ngozi yako kuonekana yenye kung’aa  na safi wakati ambapo zipo sokoni.

“Bidhaa zetu ni asili na zina ubora wa hali  ya juu kwani zimetengenezwa kwa vitu halisi ikiwemo matunda,mimea na majani ya hasili na kufanya ngozi kuwa katika hali ya afya wakati wote wa matumizi” alieleza Bwana. Piyush Chandra.

Aidha, Kilele cha maadhimisho hayo ya miaka 50 kinatarajia kufikia tamati hadi hapo Septemba mwaka huu ambapo  zaidi ya Wanafamilia  60,000 kutoka Duniani kote watakaojumuika kwenye meli kubwa ambayo ni maalum na ya kifahari watakutana pamoja na kufurahia huku miongoni mwao wakitokea Tanzania ambao ni pamoja na Mawakala wa bidhaa hizo.

Katika hatua nyingine, Oriflame Tanzania wameweza kumtangaza Balozi mpya wa bidhaa hizo hapa nchini ambapo walimtangaza Mariam ambaye anajulikana zaidi kama Miss Popular anayemiliki nna kuendesha blog ya Miss Popular inayojishughulishana na shughuli mbambali za urembo na mitindo hivyo kupitia  yeye na blog yake  watu mbalimbali watafikiwa na kuwa balozi mzuri wa bidhaa hizo.

 Oriflame (EA) Tanzania Limited ni tawi la Oriflame East Africa ambalo makao yake makuu yapo nchini Sweden. Oriflame Tanzania  kwa hapa nchini imefunguliwa Mei  mwaka 2011 huku ikiwafikia watanzania mbalimbali kwa kuwapatia ajira ikiwa ni pamoja na za uwanachama, wasambazaji, na waajiriwa wa kudumu huku malengo makuu ya Oriflame ni kuwa kampuni namba moja duniani inayofanya biashara ya vipodozi kwa namna ya mtandao (Network Marketing).

Chanzo: Na Andrew Chale-MO BLOG.

Halima Shawib kutoka Oriflame Tanzania akizungumza katika tukio hilo

Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Oriflame kwa Nchi za Afrika, Piyush Chandra akizungumza katika tukio hilo jana Juni 8.2017 Jijini Dar e s Salaam.

Balozi wa Sweden Nchini Tanzania, Bi. Katarina Rangnitt akizungumza katika tukio hilo

Mkuu wa  Masoko wa Oriflame Tanzania, Bi. Mary Riungu akizungumza katika tukio hilo jana Juni 8.2017 Jijini Dar e s Salaam.

Balozi mpya wa bidhaa hizo hapa nchini ambapo walimtangaza Mariam ambaye anajulikana zaidi kama Miss Popular akizungumza katika tukio hilo

Balozi mpya wa bidhaa hizo hapa nchini ambapo walimtangaza Mariam ambaye anajulikana zaidi kama Miss Popular akizungumza katika tukio hilo

Balozi mpya wa bidhaa hizo hapa nchini ambapo walimtangaza Mariam ambaye anajulikana zaidi kama Miss Popular akizungumza katika tukio hilo

Mdau akipozi na zawadi ya miaka 50 ya bidhaa za Oriflame. (Picha zote na ANDREW CHALE-MO BLOG).

Wadau wakipozi katika tukio hilo. Kushoto ni Mwandishi Mwandamizi wa Mtandao wa MO BLOG Andrew Chale akiwa pamoja na Mwanahabari Mwandamizi, Yamola Junior.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here