Mwigulu achimba visima 48 Jimboni kwake Iramba

0
95

Mbunge wa  Jimbo  la Iramba Magharibi , Mh. Mwigulu Mchemba ameweza kutembelea miradi ya visima vinavyochimbwa na alivyochimba visima vya maji 48 ilikutatua kero ya maji jimboni humo.

Mradi huo huo mkubwa wa kuchimba visima vya maji 48 ndani ya jimbo hilo ameufanya katika Vijiji ambavyo vinatatizo kubwa la upatikanaji wa maji kwa muda mrefi sasa.

Mradi unasimamiwa na ofisi ya mbunge wa jimbo hilo, Awali  Mh. Mwigulu Mchemba alihaidi na kwa sasa  ameshaanza utekelezaji wake wa kuchimba visima vijiji vya Kisonga, Kisonzo ,kinapanda  na vingine vingi ndani ya jimbo hilo.

Akitembelea kukagua baadhi ya visima hivyo ambavyo vinachimbwa kisasa, baadhi ya Wananchi wa maeneo ambayo visima hivyo vitachimbwa wamesema wanashukuru kwa ujio wa visima hvyo  na wataondokanana tatizo la muda mrefu la maji safi.

“Tumekuwa tukisumbuliwa na tatizo la maji safi muda mrefu. Ujio wa visima hivi ni faraja kwetu na tunampongeza Mbunge wetu kwa kutimiza ahadi yake kwetu” alieleza mmoja wa Wananchi wa jimbo hilo.

Imeelezwa kuwa, katika vijiji hivyo ambavyo kwa saasa Mbunge huyo ameelekeza nguvu zake za kuchimba visima,  maji yamekuwa yakiwasumbua sana hasa kipindi hiki wanapoelekea kiangazi huwa kuna ukame hivyo maji wanayafata umbali mrefu huku wanaopata shida kubwa ni wakinamama ambao wanalazimika kuamka asubuhi mapema kuyafata mabondeni  ambapo pia nayo yanakuwa si salama.

TAZAMA HAPA KUONA TUKIO HILO

Mwigulu akizungumza na wananchi juu ya tukio hilo

Baadhi ya mitambo ya kuchimba visima ikiendelea na shughuli zake hizo jimboni

Mwigulu akipata maelekezo kutoka kwa wakandarasi wanaochimba visima jimboni humo

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here