News Alert:Mwigulu afunga mipaka ya nchi, aagiza waliotajwa na Rais Magufuli kutosafiri

0
431

Waziri wa Mambo ya ndani ya nchi Mh. Mwigulu Nchemba usiku huu ametoa tamko zito kupitia taarifa yake fupi aliyobandika ‘post’ kwa mitandao yake maalum ya kijamii akiagiza mamlaka husika za ulinzi na usalama zilizo chini yake kuhakikisha hakuna kiongozi hata mmoja kati ya waliyetajwa leo Juni 12.2017 na

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli wakati akipokea Taarifa ya Kamati ya pili ya Uchunguzi wa Madini yaliyo kwenye makontena yenye mchanga unaosafirishwa nje ya nchi kutoka kwenye machimbo ya madini sehemu mbalimbali hapa nchini kutoka kwa Mwenyekiti wa Kamati hiyo Profesa Nehemiah Osoro Ikulu jijini Dar es Salaam ambapo aliwataja viongozi mbalimbali akitaka wachunguzwe kwa hatua zaidi.

Kupitia ukurasa huo Mh. Mwigulu aliandika: “Hakuna uzalendo zaidi ya kulinda rasilimali za Taifa, Hakuna utetezi wa wanyonge zaidi ya kulinda rasilimali zao.Hongera sana Mh.Rais kwa uzalendo wa vitendo kwa Taifa letu.

Naelekeza wote waliotajwa kuhusika hakuna kutoka nje ya mipaka ya nchi yetu isipokuwa kwa kibali maalum kutoka serikalini. Vyombo vitekeleze maagizo ya Rais kwa utimamu.” aliandika Mwigulu.

Andiko hilo la Mwigulu kupitia Twitter yake

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here