Magonjwa yaliyokuwa hayapewi kipaumbele kutokomezwa ifikapo 2020-Serikali

0
134

Serikali imejidhatiti kutokomeza magonjwa yaliyokuwa hayapewi kipaumbele ili kutimiza malengo ya kujenga uchumi wa viwanda na afya bora mpaka kufikia 2020.

Hayo yamesemwa na Mganga Mkuu wa Serikali Prof. Mohammed Kambi wakati wa ufunguzi wa mkutano mkuu wa mwaka unaolenga kupitia shughuli za mpango wa Taifa wa kudhibiti magonjwa yaliyokuwa hayapewi kipaumbele.

“Tunataka mpaka kufikia 2020 tuwe tumetokomeza magonjwa yaliyokuwa hayapewi  kipaumbele  kama mabusha na matende ili kuweza kuinusuru nchi katika aina hii ya magonjwa yanayojitokeza katika nchi zinazoendelea hususan Tanzania” alisema Prof. Kambi.

Aidha Prof. Kambi amesema kuwa licha ya kudhibiti mabusha na matende pia wamejidhatiti kuzuia ugonjwa wa usubi na kichocho kabla ya kufikia 2025 ili kuendana na mpango wa dunia wa kudhibiti magonjwa hayo.

Kwa upande wake Mratibu wa Mpango wa Taifa Wa kudhibiti magonjwa yaliyokuwa hayapewi kipaumbele Dkt. Upendo Mwingira amesema kuwa wananchi wanatakiwa wajitokeze kupata dawa na tiba za magonjwa hayo kwan hazina madhara kwa binadamu.

Mkutano huo uliokutanisha wadau mbalimbali wa sekta ya afya  kutoka duniani kote umelenga kupata mpango kazi wa kudhibiti magonjwa yaliyokuwa hayapewi kipaumbele kwa mwaka 2017 na 2018 ili kuweza kupata njia za kudhibiti magonjwa hayo kama vile mabusha na matende, kichocho na usubi.

Wadau kutoka nchi mbali mbali wakifuatilia mjadala kwa ukaribu katika mkutano wa mwaka wa mapitio ya shughuli za mpango wa Taifa wa kudhibiti magonjwa yaliyokuwa hayapewi kipaumbele uliofunguliwa na Mganga Mkuu wa Serikali Prof Bakari Kambi (Hayupo kwenye Picha) uliyofanyika Kunduchi jijini Dar Es salaam.

Mganga Mkuu wa Serikali Prof Bakari Kambi akiwasirisha mchango wake mbele ya wadau wa magonjwa yaliyokuwa hayapewi kipaumbele (Hawako kwenye picha) katika mkutano wa mwaka wa mapitio ya shughuli za mpango wa Taifa wa wa udhibiti wa magonjwa hayo uliyofanyika Kunduchi jijini Dar Es salaam.

Wadau wakifuatilia mjadala kwa ukaribu katika mkutano wa mwaka wa mapitio ya shughuli za mpango wa Taifa wa kudhibiti magonjwa yaliyokuwa hayapewi kipaumbele uliofunguliwa na Mganga Mkuu wa Serikali Prof Bakari Kambi (Hayupo kwenye Picha) uliyofanyika Kunduchi jijini Dar Es salaam.

Mratibu wa Mpango wa taifa wa magonjwa yaliyokuwa hayapewi kipaumbele Dkt Upendo Mwingira akifuatilia kwa ukaribu mjadala uliokuwa ukiwasilishwa na Mganga Mkuu wa Serikali Prof Bakari Kambi (hayupo kwenye picha) katika mkutano wa mwaka wa mapitio ya shughuli za mpango wa Taifa wa kudhibiti magonjwa yaliyokuwa hayapewi kipaumbele, anaefuatia ni Mkurugenzi wa Idara ya Afya TAMISEMI Dkt. Ntuli Kapologwe na mkurugenzi wa kinga Dkt Neema Ruzibamayila.

Meza kuu

Picha ya pamoja ya Wadau wa Magonjwa yaliyokuwa hayapewi kipaumbele ikiongozwa na Mganga Mkuu wa Serikali Prof Bakari Kambi katika mkutano wa mwaka wa mapitio ya shughuli za mpango wa Taifa wa magonjwa hayo uliyofanyika Kunduchi jijini Dar Es salaam.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here