Rais Dkt. Magufuli aonya watu wanaochafua viongozi kupitia ripoti za tume ya Makinikia

0
329

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli ametoa onyo kali kwa watu wanaochafua viongozi waliotangulia kupitia tume mbili za kuchunguza Makinikia ambapo  amefafanua kuwa, hakuna mahali popote ilipotajwa jina la Kikwete na Mkapa huku akiwataka watanzania kuacha mara moja kuwahusisha Wazee hao kwani wameifanyia mambo makubwa Tanzania.

Rais Magufuli ameyasema hayo mapema leo Juni 14, 2017 Ikulu Jijini Dar es Salaam  ambapo amekerwa na magazeti yanayotaja viongozi wastaafu kwenye sakata  hilo la madini.

Rais Magufuli ametumiwa wasaha wa kuvionya vyombo vya habari vinavyowataja Marais wastaafu akiwemo Mhe. Benjamin William Mkapa na Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete na kuwahusisha na taarifa za kamati mbili za uchunguzi wa madini yaliyo katika makontena yenye mchanga wa madini (Makinikia) ambao ripoti zimekabidhiwa kwake na kamati hizo.

“Nimesoma ripoti zote mbili hakuna mahali ambapo Mzee Mkapa na Mzee Kikwete wametajwa, vyombo vya habari viache kuwachafua hawa wazee, wamefanya kazi kubwa ya kulitumikia Taifa letu, viwaache wapumzike” amesema  Rais Magufuli.

 Chanzo: Gerson Msigwa, Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, IKULU Dar es Salaam

14 Juni, 2017

TAZAMA HAPA KUONA TUKIO HILO:

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here