Trafiki auawa Kibiti, gari lao lachomwa moto

0
296

Taarifa za kuaminika zilizolifikia gazeti  la Mwananchi zilizochapishwa kupitia mtandao  wake huo mchana wa leo  zimeeleza askari wa Usalama wa barabarani katika kijiji cha Bungu B, Wilaya ya Kibiti ameuawa na gari kuchomwa moto  huku ikieleza kuwa, vikosi vya ulinzi na usalama vinaelekea eneo la tukio.

Watu wasiojulikana wamemuua askari wa Usalama Barabarani katika Kijiji cha Bungu B wilayani Kibiti, Majira ya mchana wa leo na kisha kuchoma moto gari lake.

Mtandao huu utaendelea kuwapatia habari zaidi kutoka eneo la tukio.

Chanzo: Mwananchi Online.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here