Wapo hapa Mastaa watakao pamba WhatsappGroups Party Juni 30.2017 ndani High Spirit Lounge Dar

0
281

Tayari baadhi ya mastaa watakaojumuika pale kati kwenye ile Party iliyokuwa ikisubiriwa kwa hamu kubwa ya WhatsAppGroups Party itakayo ‘happen’ ndani ya  ukumbi wa kisasa na ‘Classic’ wa High Spirit Lounge, uliopo Posta mpya Jijini Dar e s Salaam hiyo Juni 30.2017. 

Baadhi ya Mastaa hao ni pamoja na Kala Jeremiah Lotta Molel, DJ Sam, Mustapha Hassanali,  Rommy Jones, Mwarabu Fighter (WCB),Z-Anto, Prince Amigo,Sholo Mwamba,  Ally Remtullah. Rose Kayuga, Josephat Mmasi (MR IFM),Mkali Wenu na wengine wengi.

Tiketi zimeshaanza kuuzwa  huku kwa Kinondoni zikipatikana Saloon kwa Rose Kayuga ama kwa kupiga simu kupitia  namba: 0718-942338 au 0745717532. Bei ya tiketi viti maalum- VIP 20,000/=, Kawaida  kiingilio Tsh. 10,000 huku kwa atakayenunua mapema kuanzia  sasa ni  TSH. 8,000 tu.

Aidha, Ofa maalum kwa Wasimamizi na Wamiliki wa Magroup ya WhatsApp (ADMINS) , ambao watakaoweza kununua tiketi  kuanzia tano kabla ya  Juni 30,  watapata ofa maalum ya punguzo ambapo kwa VIP- watauziwa kwa Tsh.15,000 huku kwa  kawaida kwa  bei hiyo ya 8000/=.

“WHATSAPP GROUPS PARTY, ni Party yenye heshima ambayo inasubiriwa na watu mbalimbali kwani imekidhi viwango na vigezo huku ikifanyika sehemu maalum ‘Classic’ yenye ulinzi wa na usalama wa hali juu na mazingira ya juu kabisa.

Njoo ukutane na marafiki, ukutane na mastaa ambao pia watu watapata kupiga picha mbalimbali za ukumbusho kwenye zuria jekundu ‘Red carpet’.

Baadhi ya mastaa hao

Moja ya eneo la ukumbi huo wa High Spirit Lounge

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here