DStv yatingisha Sabasaba kwa ofa kabambe na ushindi wa Banda bora!

0
123

Moja ya vinara wa Teknolojia ya Habari na mawasiliano katika Maonyesho yanayoendelea ya biashara jijiji Dar es Salaam – Multichoice Tanzania, imeendelea kutingisha katika viwanja hivyo huku Makundi ya watu wakimiminika kupata ofa maalum ya sabasaba kutoka DStv.

Multichoice Tanzania (DStv) ambao walitangazwa rasmi kuwa washindi wa pili katika kundi la washiriki wa Teknolojia ya Habari na Mawasiliano wamemwaga ofa ya aina yake ambapo gharama ya kufungiwa king’amuzi cha DStv pamoja na kifurushi cha mwezi mzima ni shilingi 69,000 tu!

Akielezea ofa hiyo Meneja Masoko wa Multichoice Tanzania Alpha Mria, amesema hii ni ofa ya aina yake kwa wateja wa ving’amuzi kwani bei hiyo ni nafuu sana na ni maalum katika msimu huu wa Sabasaba.

Amesema Mteja mpya wa DStv sasa atapata king’amuzi cha DStv, kifurushi cha Bomba cha mwezi mzima pamoja na ufundi bure kabisa! Ameongeza kuwa wameweka ofa hiyo kwa viwango tofauti ili kumuwezesha mteja kuamua anachokipenda kwani amteja anaweza kuamua kuchukua ofa ya king’amuzi kilichounganisha na kifurushi cha mwezi kwa Shilingi 69,000 au hata kwa mwaka mzima kwa shilingi 300,000.

“Ofa tulizonazo ni nyingi sana kwani pia tuna ofa ya ving’amuzi maalum vya kisasa vijulikanavyo kama Explora vyenye uwezo wa kurekodi vipindi, kupeleka mbele au kurudisha nyuma vipindi.” Alisema Alpha

Katika promosheni hii mteja atakayelipa sh.185, 000 atapata king’amuzi maalum cha Explora na kifurushi cha Compact mwezi mmoja wakati ambapo kwa sh.321, 000 mteja atapata Explora, Smart LNB, Dish na Kifurushi cha Compact mwezi pamoja na ufundi BUREE!

DStv ni moja ya ving’amuzi maarufu hapa nchini ambavyo vimekuwepo kwa takriban miaka ishirini na kujizolea umaarufu mkubwa hasa katika utoaji wa burudani, michezo, habari za elimu, biashara, jamii, sayansi, teknolojia na utafiti.

Mwishoni mwa mwaka jana, DStv ilipunguza sana gharama za vifurushi vyake ili kuwawezesha watanzania wengi zaidi kufurahia huduma zao ambapo kwa sasa kifurushi maarufu cha Bomba kinapatikana kwa Sh 19,975 tu!

Sambamba na kupunguza bei, pia DStv ilianzisha chaneli maalum yenye maudhui ya kitanzania ijulikanayo kama Maisha Magic Bongo DStv namba 160. Chaneli hii imejipatia umaarufu mkubwa sana kwani imekuwa ikirusha maudhui ya Kitanzania ikiwemo muziki, michezo ya kuigiza, filamu na tamthilia za hapa nyumbani ikiwemo tamthilia ya HUBA ambayo kwa sasa inaongoza kwa umaarufu hapa Afrika Mashariki.

l

Baadhi ya wateja wa DStv wakipata huduma mbalimbali ndani ya banda lililopo katika viunga vya Sabasaba

Baadhi ya wateja wa DStv wakipata huduma mbalimbali ndani ya banda lililopo katika viunga vya Sabasaba

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here