UBER watoa ofa ya usafiri wa bure kwa wateja wao Sabasaba

0
145

Kampuni ya huduma ya usafiri ya Uber  inayofanya shughuli zake  jijini Dar es Salaam imewakaribisha watu mbalimbali kujitokeza kujitokeza kuunganishwa na huduma hiyo ambayo imeweza kurahisisha maisha ya watu wengi kupitia usafiri ambapo mteja atakayepakua program ya Uber atapata ofa hiyo ya bure kwa safari ya kwanza.

Uber wapo nje ya banda la Wizara ya fedha na jirani ya banda la Karume katika mabanda ya Maonesho ya 41 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam (Sabasaba) yanayoendelea katika viwanja vya Mwl. Julius Kambarage Nyerere vilivyopo barabara ya Kilwa Jijini Dar es Salaam wametoa ofa hiyo kabambe ya mteja kuweza kuipakua App hiyo ya Uber kwa simu yake.

Kwa mujibu wa wataalam wa kampuni hiyo wameeleza kuwa, wateja wao wanaotembelea hapo watapata elimu mbalimbali pamoja na kufafanuliwa masuala ya kitaalam huku pia wakipata kuelekezwa namna ya kupakua program hiyo ya Uber yenye ofa ya punguzo la  Tsh. 8,200 kwa safari ya kwanza.

“Uber  kwa kipindi hiki cha Sabasaba tuna ofa maalum ya punguzo la Tsh 8,200, kwa mteja atakayejiunga sasa hivyo pesa hizo zinalipia safari yake ya kwanza. Mfano umei Uber ikupeleke sehemu ambayo ulitakiwa ulipe Ths 6,000, hapo hautolipa pesa utaenda bure. Pia kama utakuwa umeita Uber  ukataka ikupeleke kwenye umbali ambao ungetakiwa kulipa Tsh. 12,000, hapo utalipa 4,000 pekee  hii ni kwa wateja ambao watakuwa wamejiunga na ofa yetu” ameeleza Alfred Msemo  kutoka Uber.

Uber kwa Jiji la Dar es salaam imeelezwa kuwa ni miongoni mwa  jiji la 475 duniani kujiunga na mtandao huo ambao unatoa huduma ya usafiri katika majiji mbambali duniani.

Huduma ya mtandao wa Uber, huwaunganisha madereva na wasafiri kwa muda muafaka, kwa kubonyeza tu kitufe cha Uber na kuagiza usafiri ambapo gari inakufuata mahala ulipoielekeza.

Meneja wa Uber Tanzania, Alfred Msemwa  akitoa ufafanuzi kwa wateja waliotembelea banda hilo

Davis Evans wa Uber akimpatia maelezo ya namna ya kupakua programu ya Uber kwa mteja aliyetembelea banda hilo

Meneja wa Uber Tanzania, Alfred Msemwa  akitoa ufafanuzi kwa wateja waliotembelea banda hilo

Francis Kimario wa Uber akitoa maelezo kwa wateja waliopita katika banda hilo la Uber

Josephine Juma wa Uber akiwa na tuzo ya ubora walioshinda katika maonesho hayo ya Sabasaba

Meneja wa Uber Tanzania, Alfred Msemwa  akiwa na tuzo waliopata katika maonesho hayo ya Sabasaba 2017

Meneja wa Uber Tanzania, Alfred Msemwa  akitoa ufafanuzi kwa wateja waliotembelea banda hilo

Geoffrey Mabula wa Uber akitoa ufafanuzi kwa wateja waliotembelea banda hilo

Monica Mziray wa Uber akitoa ufafanuzi wa wananchi waliofika katika banda hilo

Tuzo ya Uber

Monica Mziray wa Uber akitoa ufafanuzi wa wananchi waliofika katika banda hilo

Timu ya Uber ikiwa katika viwanja hivyo vya Sabasaba  mwaka huu tayari kwa kukusaidia namna ya kutumia huduma ya usafiri wa Uber. ( Picha zote na Andrew Chale)

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here