Kigi Makasi afunga pazia la usajili Singida United FC

0
233

Tayari Klabu iliyopanda ligi Kuu mwaka huu ya Singida United imeweza kukamilisha zoezi la usajili kwa kumsajili  mchezaji Kigi Makasi, Winga huyu aliyehudumu kwa nyakati tofauti timu ya Taifa ya Tanzania, Simba S.C na baadae Ndanda Fc, anakuwa wa mwisho katika kufunga dirisha la usajili la Wanasingida.

Kigi anajiunga na Singida United  kwa uhamisho wake kutoka Ndanda Fc alipokuwa akitumikia soka lake.

Imeelezwa kuwa, Kigi ni miongoni mwa wachezaji  wenye moyo wa kujituma vilivyo awapo uwanjani, ameamua kuivia beji ya ukepteni wa Ndanda Fc na kuelekea katikati mwa nchi ya Tanzania kuungana na timu ya Ushindi SU.

Kigi Makasi amekuwa ndio mchezaji anayefunga ukurusa wa usajili ndani ya Singida United kwa msimu wa 2017/2018.

Mpaka sasa SU  imeshamaliza kufunga ukurasa wa wachezaji wa nje (7players) ambao ni pamoja na 1.Elisha Muroiwa(Zimbabwe), 2.Twafadzwa Kutinyu (Zimbabwe), 3.Simbarashe Nhivi (Zimbabwe), 4.Wisdom Mtasa (Zimbabwe), 5.Shafik Batambuze(Uganda), 6.Dany Usengimana( Rwanda) na  7.Michel Rusheshangoga(Rwanda)

Wachezaji 9 wa ndani wa SU ni pamoja na : 1.Atupele Green (Jk Ruvu), 2.Miraj Adam (Africa Lyion)

3.Kenny Ally (Mbeya City), 4.Roland Msonjo(Mshikamano Fc), 5.Pastory Athans (Simba), 7.Deus Kaseke(Yanga), 8.Ally Mustapha (Yanga) na  9.Kigi Makasi (Ndanda Fc) mbali  na hao pia inawachezaji wengine na kufanya timu hiyo kuwa na jumla ya wachezaji 25.

“Wchezaji 9 ni wale waliosalia baada ya timu kupanda kucheza Ligi Kuu Tanzania bara msimu wa 2017/2018 Na wengine waliokuwapo awali” ilieleza taarifa ya timu hiyo na kuendelea kusema kuwa:  Tunawashukuru vilabu mbalimbali ambao tulifikia makubaliano nao na wamewachukua baadhi ya wachezaji wetu walioipandisha timu, na baadhi ya wachezaji waliomba kuondoka kwa ridhaa yao.

 

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here