SMZ yavutiwa na uwekezaji wa Halotel nchini

0
131

Kamati ya Ardhi na Mawasiliano ya Baraza la Wawakilishi Zanzibar (SMZ) imevutiwa na uwekezaji uliofanya na kampuni ya simu ya Halotel hususan Visiwani Zanzibar, na kuitaka kampuni hiyo kuhakikisha inaendeleza uwekezaji wake visiwani humo sambamba na kupunguza gharama za mawasiliano kwa wakaazi wa visiwa hivyo.

Akizungumza na uongozi wa kampuni hiyo, Mwenyekiti wa Kamati ya Miundombinu na Mawasiliano ya baraza la wawakilishi la serikari ya Mapinduzi ya Zanzibar, Hamza Hassan amesema kuwa kamati yake imeridhishwa na uwekezaji uliofanywa na kampuni hiyo na kuiomba kufanya uwekezaji zaidi ili kurahisisha maisha wa wananchi.

“Tunatambua mchango wa Halotel kutokana na uwekezaji mkubwa walioufanya katika sekta ya mawasiliano, ambayo inachangia kukuza maendeleo ya nchi ya Tanzania bara na visiwani ikiwemo sekta ya ajira, teknolojia, elimu na mawasiliano katika maeneo mengi mjini na vijijini ambayo hayakuwa na huduma ya mawasiliano.” Alisema na kuongeza

“Tumefarijika sana kwa jinsi ambavyo Halotel imekuwa ikishirikiana na serikali katika kuboresha sekta ya elimu kupitia teknolojia, kwa mfano mradi huu wa kuunganisha shule zaidi ya 400 na huduma ya intaneti ni ya kipekee sana, lazima tuhakikishe sisi kama serikali tunausimamia na kuhakikisha unaleta mabadiliko, miradi kama hii ni lazima serikali iwekeze nguvu za kutosha kuhakikisha inakuwa na tija kwa elimu yetu.” Alisema

“Tunawaomba Halotel waangalie namna ya kuanzisha mfumo wa Matumizi ya Komputa kwa watoto wetu kuanzia shule za msingi, ili iwe rahisi kukabiliana na mabadiliko ya teknolojia, Mfano nchi kama ya Rwanda imefanikiwa kutoa komputa kwa wanafunzi na huduma ya intaneti natolewa katika shule nyingi, sisi tuna miradi kama hii lakini hatuipi kipaumbele katuika kuleta mapinduzi katika elimu.” Alihitimisha Hamza.

Akizungumza kwa niaba ya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Naibu waziri wa Miundombinu, Mawasiliano na Usafirishaji Mohamed Ahmada Salum, amesema kuna maeneo mengi visiwani Zanzibar ambayo bado yanakabiliwa na changamoto ya huduma bora za Mawasiliano na hivyo kampuni hiyo iangalie ni namna gani wanaweza kufikisha mawasiliano mapema iwezekanavyo.

Aidha akijibu agizo hilo, Mkurugenzi Mtendaji wa Halotel, Le Van Dai, alisema tayari wameomba kibali cha kujenga minara mipya katika maeneo ya Pemba na maeneo mengine lakini bado hawajakubaliwa na Mamlaka husika.

“Mhe. Naibu Waziri, Lengo letu ni kuhakikisha tunafikisha Mawasiliano katika maeneo yote ya nchi hii, hadi sasa tumeomba vibali kujenga maeneo mapya ya minara visiwani Zanzibar lakini bado mamlaka husika hazijatupatia vibali hivyo, tunakuahidi kuwa mapema tu tutakapo fanikiwa kupata vibali hivyo tutahakikisha tunafikisha mawasiliano katika maeneo ambayo bado yana changamoto.” Alisema Dai.

“Hadi sasa sasa Kampuni yetu imekwisha jenga miundombinu  ya mawasiliano kwa kujenga minara ya mwasailiano zaidi ya 42000 (BTS), na Zaidi ya kilomita 20,000 za mkongo wa taifa na mawasiliano (Fiber cable) na kuunganisha vijiji zaidi ya 3000 ambavyo vilipata huduma ya Mawasilaino kwa mara ya kwanza.” Alihitimisha Dai.s

Kwa upande wake, Naibu waziri wa ardhi Juma Makungu, Alisema kuwa wao kama wawakilishi wa serikali watahakikisha wanajemba mazingira rafiki kwa kampuni hiyo kufanya uwekezaji katika maeneo ambayo hayajafikiwa na mawasiliano.

Kamati ya Ardhi na Mawasiliano ya Baraza la wawakilishi Zanzibar, imefanya ziara ya kujifunza katika kampuni hiyo ikiwa imeambatana na wajumbe pamoja na watendaji wa sekta mbalimbali za Mawasiliano na ardhi ili kuhakikisha inajenga fursa ya wawekezaji Zaidi katika teknolojia ya Mawasiliano.

Mkurugenzi Mtendaji wa Halotel, Le Van Dai (wa kwanza kushoto) akitoa maelezo namna teknolijia ya kufanya vikao kupitia Video (Video conference) jinsi inavyofanya kazi kwa Mwenyekiti wa Kamati ya Miundombinu na Mawasiliano ya baraza la wawakilishi la serikari ya Mapinduzi ya Zanzibar Hamza Hassan,(Wa kwanza kulia) Naibu waziri wa Miundombinu Mawasiliano na Usafirishaj,  Mohamed Ahmada Salum, (Katikati), viongozi hao pamoja na kamati ya Miundombinu na Mawasiliano ya Baraza la Wawakilishi walitembelea ofisi za kampuni hiyo kwa ajili ya kujifunza na kuangalia fursa Zaidi za uwekezaji visiwani Zanzibar.

Mkurugenzi Mtendaji wa Halotel, Le Van Dai (wa kwanza kushoto) akiulizwa swali na Wajumbe Kamati ya Miundombinu na Mawasiliano ya baraza la wawakilishi la serikari ya Mapinduzi ya Zanzibar  wakatiwa wa tukio hilo la maelezo namna teknolijia ya kufanya vikao kupitia Video (Video conference) jinsi inavyofanya kazi

Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano wa Halotel, Mhina Semwenda akitoa maelezo mbele ya Kamati ya Ardhi na Mawasiliano ya Baraza la Wawakilishi Zanzibar (SMZ), namna kampuni hiyo ilivyofanya uwekezaji katika kufikisha huduma za mawasiliano vijijini, na Ushirikiano kati ya kampuni hiyo na Serikali uliowezesha zaidi ya 400 kufikiwa na huduma za intaneti kamati hiyo ilitembelea ofisi za kampuni hiyo kwa ajili ya kujifunza na kuangalia fursa Zaidi za uwekezaji visiwani Zanzibar.

Mkurugenzi Mtendaji wa Halotel, Le Van Dai (wa kwanza kulia) pamoja na Mshauri wa Kampuni hiyo Balozi Fransis Mndolwa, wakitoa maelezo kwa Kamati ya Miundombinu na Mawasiliano ya baraza la Wawakilishi la serikari ya Mapinduzi ya Zanzibar namna ambavyo kampuni ya simu ya Halotel imejidhatiti katika  kuhakikisha inaendelea kusambaza huduma za mawasiliano kwa Tanzania bara na Visiwani, kamati hiyo ilitembelea ofisi za kampuni hiyo kwa ajili ya kujifunza na kuangalia fursa Zaidi za uwekezaji visiwani Zanzibar.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here