Siku ya Wahandisi Kufanyika Dodoma Septemba 7 na 8

0
101

MAADHIMISHO ya Siku ya Wahandisi Tanzania kwa mwaka 2017 yanatarajiwa kufanyika mjini Dodoma huku yakiambatana na shughuli mbalimbali za uhandisi ikiwemo kuwatambua na kuwazawadia waandisi waliofanya vizuri katika taaluma yao. Akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam Msajili wa Bodi ya Wahandisi, Mhandisi Patrick Barozi alisema miongoni mwa shughuli ambazo zitafanyika katika siku hiyo ni pamoja na mijadala na mada za kitaaluma, kiapo cha wahandisi wataalamu, maonesho ya kiufundi na biashara.
m
Mhandisi Barozi alisema mada zitakazotolewa katika jumuiya ya wahandisi ni pamoja na Jukumu la Elimu kwa ajili ya maendeleo ya viwanda nchini, maendeleo ya ujuzi/ufundi, ubunifu, masoko, ujasiriamali na umuhimu, masuala ya mazingira na maendeleo ya viwanda nchini, uimara wa afya na nyingine nyingi.

Aidha aliongeza kuwa moja ya madhumuni ya maadhimisho ya wahandisi ni kuiwezesha jumuiya ya wahandisi kuiuonesha jamii kile ambacho wahandisi wa kitanzania wanaweza kufanya katika kuleta maendeleo ya nchi pamoja na ubunifu mbalimbali waliofanywa na wahandisi wa kitanzania.

Alisema miongoni mwa taasisi ambazo zitaonesha ubunifu wa kiufundi ni pamoja na Chuo Kikuu cha Uandisi na Teknolojia (CoET), Taasisi ya Teknolijia ya Dar es Salaam (DIT), Chuo Kikuu cha Uhandisi na Teknolojia St. Joseph (SJUIT), Chuo Kikuu cha Ardhi (ARU), Makandarasi mbalimbali, kampuni za ushauri wa kihandisi, na nyinginezo.

“…Kama ilivyokuwa miaka ya nyuma…Siku ya Wahandisi ni dhahiri kuwa ni tukio linalowakusanya pamoja wahandisi wengi wa fani mbalimbali. Kwa kuzingatia hilo, Bodi inapenda kualika mashirika, taasisi na wafanyabiashara mbalimbali kutumia fursa hii kuonesha biadhaa zao,” alisema Mhandisi Patrick Barozi na kuongeza kuwa mada kuu ya maadhimisho ya mwaka huu ni ” Mchango wa Sayansi, Teknolojia, Uhandisi na Hisabati katika kuendeleza viwanda nchini”.

 

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here