Waziri wa Tanzania apoteza ndugu 13 wa familia moja kwenye ajali ya gari Kampala,Uganda

0
845

Aliyewahi kuwa Waziri katika Serikali iliyopita Gregory Teu ambaye pia alikuwa Mbunge wa Mpwapwa, Mkoani Dodoma, amepoteza ndugu wa familia yake hiyo kufuatia ajali mbaya ya gari iliyotokea usiku wa kuamkia leo Septemba 18,2017, Kampala Uganda.

Taarifa zinaeleza kuwa, ajali hiyo mbaya iliyosababisha vifo  vya watu zaidi ya 13 na kujeruhi wengine kadhaa ikihusisha gari yenye namba T 540 DLC, tukio lililotokea karibu na mto Katonga, barabara ya Masaka usiku wa kuamkia leo tarehe 18/09/2017.

Gari hilo lilikuwa likiwarudisha watu hao ambao ni  Watanzania wa familia ya Naibu Waziri huyo aliyekuwa akiyumikia Wizara yaViwanda na Biashara, Bw Gregory Teu ambapo imeelezwa familia hiyo ilikuwa nchini humo  kwenye harusi  iliyofanyika Septemba 16, mwaka huu, Kampala.

Imeelezwa kuwa,  Bibi harusi ni mtoto wa Bw na Bibi Gregory Teu mkazi wa Dar es salaam.

“Jumla ya abiria waliokuwa kwenye gari ni abiria 19. Kati yao 13 wamefariki dunia na 6 wamelazwa Nsambya hospital. Ubalozi unaendelea kufuatilia msiba huu pamoja na kupata majina yote ya waliokufa na kunusurika.

Tayari Naibu Balozi Mh. Maleko pamoja na Brigedia Generali S S Makona wameelekea Nsambya Hospital kuona walio nusurika” kilieleza chanzo cha Ofisi ya Ubalozi, Uganda.

Watanzania 13 wa familia ya Gregory Teu, wafariki katika ajali nchini Uganda==========================================Watu 13 wamepoteza maisha na wengine kadhaa wamejeruhiwa katika ajali ya gari iliyotokea Katonga wilayani Mpiji nchini Uganda.Ofisa wa polisi wa Katonga, Philip Mukasa amesema ajali hiyo imetokea usiku wa kuamkia leo Jumatatu ikihusisha basi aina ya Toyota Coaster lililogongwa na lori.Mukasa amesema basi lililohusika katika ajali hiyo lina namba ya usajili ya Tanzania na lori lina namba za Uganda.Amesema lori lililokuwa katika mwendokasi lilipasuka gurudumu hivyo kuyumba na kugonga gari hilo la abiria. —Tangazo la Ajali ya Gari TZ 540 DLCGari tajwa hapo juu lilipata ajali karibu na mto Katonga, barabara ya Masaka kuamkia leo tarehe 18/09/2017.Lilikuwa likiwarudisha Watanzania wa Familia ya Bw Gregory Teu ambao walikuja kwenye harusi tarehe 16/09/2017 hapa Kampala. Bibi harusi ni mtoto wa Bw na Bibi Gregory Teu wa Dar es salaam.Jumla ya abiria waliokuwa kwenye gari ni abiria 19. Kati yao 13 wamefariki dunia na 6 wamelazwa Nsambya hospital.Ubalozi unaendelea kufuatilia msiba huu pamoja na kupata majina yote ya waliokufa na kunusurika.Naibu Balozi Mh. Maleko pamoja na Brigedia Generali S S Makona wameelekea Nsambya Hospital kuona Walio nusurika.Asante sanaOfisi ya Ubalozi

Posted by Sadick Hamidu on Monday, September 18, 2017

Baadhi ya majina ya waliopoteza maisha kwenye ajali hiyo

Eneo la ajali hiyo linavyoonekana

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here