Rais Magufuli awaapisha Mawaziri,Manaibu Mawaziri na Katibu wa Bunge, aongoza Baraza la Mawaziri

0
228

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli leo tarehe 09 Oktoba, 2017 amewaapisha Mawaziri 8, Naibu Mawaziri 16 na Katibu wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, aliowateua tarehe 07 Oktoba, 2017.

Mawaziri walioapishwa ni George Huruma Mkuchika – Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Selemani Said Jafo – Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Dkt. Charles John Tizeba – Waziri wa Kilimo, Luhaga Joelson Mpina – Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Dkt. Medard Matogoro Chananja Kalemani – Waziri wa Nishati, Anjellah Kairuki – Waziri wa Madini, Dkt. Hamis Andrea Kigwangalla – Waziri wa Maliasili na Utalii na Mhandisi Isack Aloyce Kamwelwe – Waziri wa Maji na Umwagiliaji.

Manaibu Waziri walioapishwa ni Joseph Sinkamba Kandege – Naibu Waziri Ofisi ya Rais TAMISEMI, George Joseph Kakunda – Naibu Waziri Ofisi ya Rais TAMISEMI, Kangi Alphaxard Lugola – Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira, Stella Alex Ikupa – Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu (Walemavu), Dkt. Mary Machuche Mwanjelwa – Naibu Waziri wa Kilimo, Abdallah Hamis Ulega – Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi.

Mhandisi Atashasta Justus Nditiye – Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano na Elias John Kwandikwa – Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano.

Manaibu Waziri wengine walioapishwa ni Subira Hamis Mgalu – Naibu Waziri wa Nishati, Stanslaus Haroon Nyongo – Naibu Waziri wa Madini, Josephat Ngailonga Hasunga – Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhandisi Stella Martin Manyanya – Naibu Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji.

William Tate Ole Nasha – Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi, Teknolojia na Ufundi, Dkt. Faustine Engelbert Ndugulile – Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Juliana Daniel Shonza – Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo na Jumaa Hamidu Aweso – Naibu Waziri wa Maji na Umwagiliaji.

Aidha, Mhe. Rais Magufuli amemuapisha Steven Nzohabonayo Kagaigai kuwa Katibu wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Pamoja na kuapishwa katika nyadhifa hizo, Mawaziri, Manaibu Waziri na Katibu wa Bunge wamekula kiapo cha uadilifu kwa viongozi wa umma kilichoongozwa na Kamishna wa Maadili, Jaji Mstaafu Harold Nsekela.

Hafla ya kuapishwa kwa viongozi hao imefanyika Ikulu Jijini Dar es Salaam na kuhudhuriwa na Makamu wa Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan, Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa, Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Job Yustino Ndugai, Jaji Mkuu wa Tanzania Mhe. Prof. Ibrahim Hamis Juma, Mwanasheria Mkuu wa Serikali Mhe. George Mcheche Masaju, Mawaziri na Makatibu Wakuu wa Wizara mbalimbali, Wajumbe wa Tume ya Utumishi wa Bunge na Kamati za kudumu za Bunge, viongozi wakuu wa vyombo vya Ulinzi na Usalama na Viongozi wa madhehebu ya Dini na vyama vya siasa.

Mara baada ya kuapishwa Mawaziri na Manaibu Waziri wamekabidhiwa nyaraka za kazi na kuanza kazi kwa kuhudhuria Kikao Maalum cha Baraza la Mawaziri kilichoongozwa na Mwenyekiti wake Mhe. Rais Magufuli.

Gerson Msigwa

Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, IKULU

Dar es Salaam

09 Oktoba, 2017

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimuapisha Bi. Angela Kairuki kuwa Waziri wa Madini Ikulu jijini Dar es salaam leo Oktoba 9, 2017

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimuapisha Dkt. Hamisi Kigwangwallah  kuwa Waziri wa Maliasili na Utalii  Ikulu jijini Dar es salaam leo Oktoba 9, 2017

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimuapisha  Mhe. Suleiman Saidi Jafo  kuwa Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais (Tawala za mikoa na Serikali za Mitaa) Ikulu jijini Dar es salaam leo Oktoba 9, 2017

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimuapisha Mhe. Kangi Lugola kuwa Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira)  Ikulu jijini Dar es salaam leo Oktoba 9, 2017

wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimuapisha Dkt Mary Machuche Mwanjelwa kuwa Naibu Waziri wa Kilimo Ikulu jijini Dar es salaam leo Oktoba 9, 2017

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimuapisha Mhe. Stella Alex Ikupa kuwa Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu (Watu wenye ulemavu)  Ikulu jijini Dar es salaam leo Oktoba 9, 2017

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimuapisha Mhe. Juliana Shonza  kuwa Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Wasanii na Michezo Ikulu jijini Dar es salaam leo Oktoba 9, 2017

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimuapisha Mhe. Stephen Kagaigai kuwa Katibu wa Bunge Ikulu jijini Dar es salaam leo Oktoba 9, 2017

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli, Makamu wa Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan, Waziri Mkuu Mhe. Kassima Majaliwa, Jaji Mkuu Profesa Ibrahim Juma, Spika wa Bunge Mhe. Job Ndugai Ikulu, Mwanasheria Mkuu wa Serikali George Masaju na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi katika picha ya kumbukumbu na Mawaziri na Naibu Mawaziri baada ya hafla ya kuapishwa  jijini Dar es salaam leo Oktoba 9, 2017

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akipeana mikono na aliyekuwa  Katibu wa Bunge Dkt. Thomas Kashilila huku Jaji Mkuuijini Dar es salaam leo Oktoba 9, 2017

 Profesa Ibrahim Juma na Mhe. Stephen Kagaigai Katibu wa Bunge mpya wakiangalia mara baada ya picha za pamoja kupigwa  Ikulu jijini Dar es salaam leo Oktoba 9, 2017

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiendesha kikao cha Baraza la Mawaziri mara tu baada ya kuwaapisha Mawaziri na Naibu Mawaziri wapya  Ikulu jijini Dar es salaam leo Oktoba 9, 2017

 

wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. January Makamba ba`ada ya Mawaziri na Naibu Mawaziri wapya  kuapishwa Ikulu jijini Dar es salaam leo Oktoba 9, 2017

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais (Utumishi) Mhe. George Mkuchika huku Makamu wa Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan, Waziri Mkuu Mhe. Kassima Majaliwa na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi wakiangalia baada ya hafla ya kuapishwa  Mawaziri na Naibu Mawaziri Ikulu jijini Dar es salaam leo Oktoba 9, 2017

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na Naibu  Waziri wa Nchi Ofisi Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe.Kangi Lugola huku  Makamu wa Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan, Waziri Mkuu Mhe. Kassima Majaliwa na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi wakiangalia baada ya hafla ya kuapishwa  Mawaziri na Naibu Mawaziri Ikulu jijini Dar es salaam leo Oktoba 9, 2017

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na Naibu Waziri wizara ya Nishati Mhe. Subira Hamisi Mgalu huku Makamu wa Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan, Waziri Mkuu Mhe. Kassima Majaliwa na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi wakiangalia baada ya hafla ya kuapishwa  Mawaziri na Naibu Mawaziri Ikulu jijini Dar es salaam leo Oktoba 9, 2017

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na Naibu Waziri wa Kilimo Dklt. Mary Mwanjelwa huku Makamu wa Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan, Waziri Mkuu Mhe. Kassima Majaliwa na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi wakiangalia baada ya hafla ya kuapishwa  Mawaziri na Naibu Mawaziri Ikulu jijini Dar es salaam leo Oktoba 9, 2017

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na Naibu Waziri  Mifugo na Uvuvi Mhe. Abdallah Ulega  huku Makamu wa Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan, Waziri Mkuu Mhe. Kassima Majaliwa na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi wakiangalia baada ya hafla ya kuapishwa  Mawaziri na Naibu Mawaziri Ikulu jijini Dar es salaam leo Oktoba 9, 2017

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na Naibu Waziri wa Maji na Umwagiliaji Mhe. Jumaa Hamidu Aweso huku Makamu wa Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan, Waziri Mkuu Mhe. Kassima Majaliwa na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi wakiangalia baada ya hafla ya kuapishwa  Mawaziri na Naibu Mawaziri Ikulu jijini Dar es salaam leo Oktoba 9, 2017

 

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na  Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu (Watu wenye ulemavu) Mhe. Stella Alex Ikupa huku Makamu wa Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan, Waziri Mkuu Mhe. Kassima Majaliwa na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi wakiangalia baada ya hafla ya kuapishwa  Mawaziri na Naibu Mawaziri Ikulu jijini Dar es salaam leo Oktoba 9, 2017

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na  Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Wasanii na Michezo Mhe. Juliana Shonza huku Makamu wa Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan, Waziri Mkuu Mhe. Kassima Majaliwa na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi wakiangalia baada ya hafla ya kuapishwa  Mawaziri na Naibu Mawaziri Ikulu jijini Dar es salaam leo Oktoba 9, 2017

 

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na  Naibu Waziri wa Kazi, Vijana na Ajira, Mhe. Anthony Mavunde   huku Makamu wa Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan, Waziri Mkuu Mhe. Kassima Majaliwa na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi wakiangalia baada ya hafla ya kuapishwa  Mawaziri na Naibu Mawaziri Ikulu jijini Dar es salaam leo Oktoba 9, 2017

PICHA ZOTE NA IKULU

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here