Kocha Simba SC aachia ngazi, viongozi wa Simba kutoa tamko

0
427

Leo Oktoba 18,2017, tayari Kaimu  kocha wa Wekundu wa Msimbazi, Simba SC, Jackson Mayanja ameweka wazi kuwa ameachana na kikosi hicho ambacho hadi sasa kimeshacheza michezo 6 huku ikiwa na pointi 12, juu kwa idadi ya magoli ya kufunga 11, dhidi ya vinara wengine Yanga na Mtibwa ambao wote wana pointi 12 na idadi sawa ya magoli  pamoja na michezo.

Licha ya kutoweka wazi sababu za kiufundi,imeelezwa kuwa,  Mayanja ameamua kukaa kando kutokana na masuala yake binafsi. Hata hivyoakizungumza kwa njia ya simu na Mtandao wa MO Blog ilivyowasiliana na msemaji wa Simba Haji Manara, umeeleza kuwa, hakuwa tayari kuzungumza baada ya kusema kuwa yupo Hospitali hata hivyo alipotafutwa mmoja wa viongozi wa Simba ambaye hakutaka  jina lake kutajwa amesema kuwa wapo kwenye kikao cha ndani na watatoa tamko rasmi.

“Tunaendelea na kikao. Habari hizo za Mayanja na sisi tumezisikia kama ulivyozikia wewe. Kwa sasa tunakutana na tutatoa tamko letu” alieleza kiongozi huyo ambaye pia ana ushawi mkubwa ndani ya Simba.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here