Manjano Beauty Academy yatoa wahitimu 120 wa masuala ya urembo

0
359

Manjano Beauty Academy mnamo Novemba 18,2017,kimetunuku Astashahada (Certificates) na Stashahada (Diploma) kwa wahitimu 120 wa kwanza wa chuo hicho katika nyanja ya urembo na utengenezaji wa nywele.

Urembo na mitindo ni moja kati ya sekta zinazoajiri mamilioni ya wanawake kwa sasa, lakini bado sekta hiyo imeendelea kuwa isiyo rasmi.

Wanawake wengi wanaofanya kazi kwenye saluni hawana utaalamu, lakini ndiyo wanaofuatwa na wanaume na wanawake kwa ajili ya kutengenezwa mionekano inayovutia, wanaishi kwa kufanya kazi kubahatisha.

Akizungumza kwenye mahafali ya kwanza ya  Manjano Beauty Academy iliyofanyika jijini Dar es Salaam, mwanzilishi wa Manjano Beauty Academy, Shekha Nasser alisema kuwa maono hayo ndiyo yaliyosababisha yeye kuanzisha Manjano Beauty Academy.

Manjano Beauty Academy ni shule kwa ajili ya afya na urembo ambayo ina lengo la kuwawezesha wasichana wa Kitanzania.

“Tunashauri, tunatoa mafunzo na kuwaandaa wanafunzi kwa ajili ya soko kwa kuwapatia ujuzi unaohitajika. Serikali haiwezi kuwaajiri wahitimu wote, hata sekta binafsi haiwezi kwa hivi sasa, kwa hiyo mafunzo haya yanawasaidia wasichana wadogo kuweza kujitengenezea soko kwenye sekta ya urembo,” alisema Shekha.

Kwa mujibu wa Shekha, wasichana hao wamekuwa wakipewa mafunzo na wakufunzi bora wanaopatikana katika sekta ya urembo  ambayo yatawatasaidia wao kutimiza malengo yao binafsi pamoja na malengo ya kitaasisi.

 “Naamini kuwa wahitimu hawa watabadilisha sekta ya urembo hapa nchini, kama Malaysia na Filipino wanavyotambulika kwa kuwa na bidhaa bora za ngozi na wataalam wa matibabu wenye weledi, huko mbeleni Tanzania itajulikana ni nchi inayotoa bidhaa bora za urembo kwa ngozi za Kiafrika, kuanzia bidhaa za urembo wa uso zinazozalishwa kwa majani ya baharini Zanzibar mpaka bidhaa za poda ambazo zina virutubisho vya asili na vyakutosha,” alisema Shekha ambaye pia ni mwanzilishi wa Sheer Illusion.

Mwaka 2015, kupitia bidhaa za LuvTouch Manjano, Shekha alizindua kampeni inayoitwa Manjano Dream Makers iliyokuwa na lengo la kuwawezesha wasichana wenye mafunzo ya kijasiriamali kujikwamua kiuchumi.

“Katika miaka miwili tangu kuanzishwa kwa taasisi ya Manjano, mtandao wa wanawake wa Manjano Dream-Makers umeweza kuenea katika majiji na miji Saba nchini na kuwasaidia kutengeneza ajira na kutengeneza kipato kwa kuuza bidhaa zao kupitia mfumo wa nyumba kwa nyumba kwa wanawake wasio na ajira,” alisema Shekha.

Aliongeza kuwa, “Leo tunajivunia kuwa na wasichana 360 ‘Manjano Dream-Makers’ wenye matumaini ya kuboresha maisha yao na familia zao kwa kuuza bidhaa za LuvTouch Manjano.”

Alisema,” Hivi sasa tuna furaha kuwa na kundi hili la mwaka 2016-2017 na wanafanya vizuri tayari kwenye soko, malengo yetu ni kutoa mafunzo kwa wasichana wapatao 5000 nchi nzima katika miaka 5 ijayo.”

Kwenye awamu mbili zilizopita, taasisi hii iliweza kutoa mafunzo kwa wasichana wa mikoa ya Dar es Salaam, Zanzibar, Mwanza, Arusha, Mbeya, Dodoma na Mtwara huku mikoa mingine ikitarajiwa kufikiwa katika awamu zijazo.

Wahitimu wakiwa katika tukio hilo

Wahitimu wakiwa kwenye picha ya pamoja na Mkurugenzi wa chuo cha Manjano Beauty Academy Shekha Nasser na mgeni rasmi mkuu was wilaya ya Ilala Sophia Mjema.

 

Mkuu wa wilaya ya Ilala Bi.Sophia Mjema akimkabidhi cheti muhitimu katika tukio hilo. pembeni ni Mkurugenzi wa chuo cha Manjano Beauty Academy Shekha Nasser  

Kuhusu Taasisi ya Manjano

Manjano ni taasisi ya kiuwezeshaji kiuchumi iliyo chini ya kampuni ya Shear Illusion Ltd,  ambayo ni msambazaji wa bidhaa za biashara ya urembo wanaohusika na urembo, bidhaa za urembo wa nywele, vitu vya ziada (accessories) na vipodozi (make-up).

Taasisi hii pia ina lengo la kuwawezesha wanawake kujikwamua kiuchumi, kwa kuwapa mafunzo yanayohusu ujasiriamali, biashara, usimamizi wa fedha, mazungumzo ya uhamasishaji, kutengeneza wajasiriamali vijana huku pia ikisambaza bidhaa za urembo za LuvTouch.

Manjano Beauty Academy

Manjano Beauty Academy ni mradi wa shule unaoendeshwa na Taasisi ya Manjano. Manjano Beauty Academy inatoa elimu bora kwa wanafunzi wa leo kwa ajili ya kutengeneza wataalamu wa kesho.

Kozi ya utaalamu wa urembo inasaidia kumfunua mwanafunzi kuhusu elimu ya urembo, ikiwapa fursa wanafunzi kupata maarifa na kuelewa namna ambavyo tasnia ya urembo inavyokwenda.

Kwa kozi nzima misisitizo umewekwa zaidi katika kuongeza sifa za wanafunzi kuweza kuajirika na mtazamo unaomvutia karibu na kila mwajiri, huku ikizalisha wanafunzi wenye uzoefu tayari kwa wigo mpana na bidhaa na mbinu ili kuchagiza wanafunzi hao kuimarika kiweledi ndani ya tasnia.

Kwa asilimia kubwa ya kozi hii muda unaangalia msingi wa upande wa nadharia wa kozi husika.

Kuhusu Manjano Dream-Makers

Taasisi ya Manjano ilianzisha mradi wake mkubwa wa kuwawezesha wasichana kiuchumi; mradi huu ulitumia njia za kibiashara ambazo zinatengeneza ajira, zinasaidia kuondoa umaskini na wakati huo huo zinaboresha vipato vya wanufaika wa mradi.

Njia hii ya kibiashara inachangia katika kuwawezesha wasichana wasio na ajira na wanaoishi maeneo ya vijijini katika kupamba na changamoto za kiuchumi na kijamii. Taasisi ya Manjano inatoa mafunzo bure kwa wanawake

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here