Ofisi ya Makamu wa Rais yakana kutoa mikopo kupitia Samia Habari Suluhu

0
196

Ofisi ya Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
inakanusha taarifa inayosambaa katika Mitandao ya Kijamii kuhusu Taasisi
ya Kiraia ijulikanayo kama Samia Habari Suluhu. Taasisi hiyo
inajitambulisha kuwa inatoa mikopo ya fedha taslim, pikipiki na bajaji kwa
wanawake wajasiriamali kwa masharti ya kuweka dhamana ya fedha
taslimu shilingi laki mbili. Ofisi inapenda kuujulisha umma kuwa taarifa hizo
ni za uongo na uzushi na zina lengo la kuupotosha umma wa Watanzania.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa
Samia Suluhu Hassan, hamiliki taasisi yoyote ya aina hiyo na hahusiki kwa
namna yoyote na kazi za taasisi hiyo na wala haitambui taasisi hiyo.
Ofisi ya Makamu wa Rais inawataka Wananchi kuzipuuza taarifa hizo
zinazosambaa kwenye mitandao ya kijamii kwani zinalenga kuleta taharuki
na kupotosha Umma wa Watanzania.
Imetolewa na:
Ofisi ya Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Ikulu- Dar es Salaam
20 Novemba, 2017.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here