Makamu wa Rais Samia awasili Nairobi kumwakilisha Rais Magufuli uapisho wa Kenyatta

0
68

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan leo asubuhi tarehe 28 Novemba, 2017 amewasili Mjini Nairobi nchini Kenya ambako anamwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli katika sherehe za kuapishwa kwa Rais wa Jamhuri ya Kenya Mhe. Uhuru Kenyatta.

Katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Jomo Kenyatta Mhe. Samia Suluhu Hassan ambaye ameambatana na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Dkt. Suzan Kolimba amepokelewa na Mhe. Balozi Robinson Njeru Githae wa Kenya na Balozi wa Tanzania nchini Kenya Mhe. Dkt. Pindi Chana.

Sherehe za kuapishwa kwa Mhe. Rais Uhuru Kenyatta zinafanyika katika uwanja wa Moi Kasarani Mjini Nairobi.

Gerson Msigwa

Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, IKULU

Nairobi

28 Novemba, 2017

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here