Naibu Waziri wa Afya Ndungulile,DC Kigamboni wathibitisha ushiriki wao Kigamboni Marathon,Desemba 2

0
239

Zikiwa zimebaki siku mbili tu kufanyika kwa mara ya kwanza mbio Kigamboni Marathon kwa mwaka 2017, tayari viongozi mbalimbali wa mashirika na taasisi za Kiserikali na binafsi wamethibitisha kushiriki mbio hizo ambazo pia zitaambatana na zoezi la Upimaji wa afya katika kuadhimisha siku ya Ukimwi Duniani ambayo huazimishwa tarehe 1 mwezi wa 12 kila mwaka na kisha mbio hizo hiyo Desemba 2, katika viunga vya Mji wa Kigamboni.

Akizungumza na mtandao huu , Ndg. Dimo Debwe Mitiki Mkurugenzi wa Events World amebainisha kuwa, maandalizi yote yanaenda sawa na wapo katika hatua mbalimbali huku watu wakiendelea kujiandikisha hii n pamoja na viongozi wa Serikali, binafsi pamoja na Mabalozi waliopo hapa nchini.

“Tunashukuru kwa sapoti tunazopewa na wadau. Tunaendelea na zoezi la uandikishaji washiriki wa mbio hizi. Hadi sasa viongozi wa Serikali waliojiandikisha ni pamoja na Naibu Waziri wa Afya, Mandeleo ya Jaamii, Jinsia, Wazee na Watoto, ambaye pia ni Mbunge wa Kigamboni Mh. Dk. Faustine Ndungulile, Mkuu wa Wilaya ya Kigamboni na viongozi wengine wengi” alieleza Dimo Debwe.

Aliongeza kuwa, lengo kuu la  mbio hizo ni kutangaza fursa za uwekezaji, vivutio vya kitalii na Biashara zilizopo Kigamboni kwa maendeleo ya Taifa zima la Tanzania na watu wake.

Pia alieleza kuwa, fomu za Usajili wa Kigamboni Marathon zinapatikana vituo vyote vya Mafuta na supermarket za TSN, Ferry Wakala wa Pesa Mtandao(Lilipo Bango, Getini kabisa) PCMC HOSPITAL – Kibada, ABSOLUTE SECURITY Mbuyuni (karibu na Liquid Bar), JPM HOSPITAL – Magomeni Kagera.

Vituo vingine vinavyopatikana fomu hizo ni Colloseum Gym (O’BEY /Masaki) New Mzalendo Gym – Toangoma, Stationary – Ofisi za Mkuu wa Wilaya ya Kigamboni, Mji Mwema na Kwa Mwenyekiti wa Jogging Clubs za Kigamboni.

Dimo Debwe amemalizia kwa kueleza kuwa, kwa watu walio mbali wanaweza kuja ushiriki wao kupitia tovuti ya www.kigambonimarathon.com

“Explore, Have Fun & Run For Healthy.. “

#KigamboniMarathon

Mkuu wa Wilaya ya Kigamboni  Hashim Mgandilwa 

Mkurugenzi Mkuu wa TSN Group Tanzania, Bwana Farouk amethibitisha kushiriki Kigamboni Marathon Jumamosi Hii 2/12/2017.

Naibu Waziri wa Afya na Mbunge wa Kigamboni Mh.Dk. Faustine Ngungulile akikabidhiwa fulana ya Kigamboni Marathon wakati wa kujaza fomu ya ushiriki 

 

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here