Kampuni ya SBC Tanzania waja na ‘JISHINDIE MAMILIONI’ kwa kunywa soda za Pepsi

0
268

Kampuni ya SBC Tanzania  Limited, watengenezaji na wasambazaji wa vinywaji  baridi aina ya Pepsi, Mirinda, 7UP, Mountain Dew na Everest  mapema leo Desemba 4, 2017, wametambulisha rasmi shindano litakalojulikana kwa jina la “JISHINDIE MAMILIONI”  ambapo litahusisha  soda aina ya Pepsi, Mirinda Orange, Mirinda Fruity, Mirinda Green  Apple, Mountain  Dew (300ml) na Seven Up za ujazo wa milioni 350 tu.

Akizungumza na vyombo vya habari jijini Dar e s Salaam, leo Desemba 4, Meneja Mafunzo na Uwezeshaji Bw.Rashid Chenja amesema watu mbalimbali watajishindia zawadi ikiwemo fedha taslimu pamoja na kinywaji cha Pepsi.

“Shindano hili la Jishindie Mamilioni ni kwa mikoa ya Dar es Salaam,  Pwani, Morogoro, Dodoma, Tanga , Lindi na Mtwara. Mteja atakayenunua kinywaji chenye vizibo vya rangi ya silva. Moja ya zawadi hizo ni pamoja na zawadi taslimu kiasi cha shilingi 1000/=, 5,000,10,000, 500,000, na kiasi cha Tsh. 1,000,000. Pia zawadi hizo kuna kujishindia soda ya bure” alieleza  Chenja.

Aliongeza kuwa, zawadi hizo,  mteja atatakiwa kubandua ndani ya kizibo na kukuta maandishi hayo ya zawadi tofautitofauti.

“vizibo vyote vya rangi ya dhahabu ndivyo vyenye zawadi katika shindano  letu. Zawadi za papo hapo  utapewa uliponunua soda dukani, Gari ya mauzo au muuzaji wa jumla. Zawadi hizo ni pamoja na Shilingi  10,000, au shilingi 5000  au kiasi cha Shilingi 1000 au soda ya bure.

..Kwa zawadi kubwa kuanzia Shilingi 1,000,000 au 500,000  fedha hizi zitakuwa zikitolewa kila siku kuanzia saa nne asubuhi hadi saa 9 jioni siku za Jumatatu mpaka Ijumaa kwa siku za kazi pekee tukio ambalo litakuwa likifanyika makao makuu ya SBC Dar  barabara ya Nyerere,  Depot ya Morogoro na  Lindi na ile ya Depot ya Dodoma.” Alieleza Chenja.

Kwa upande wake Meneja Masoko wa Pepsi, Roselyne Bruno alieleza kuwa shindano hilo ni fursa nzuri kwa wanywaji wa soda za kampuni hiyo kujishindia mamilioni kila siku kwa kunywa Soda zao.

“Kila siku mteja atakayenunua bidhaa zetu anayo nafasi ya kujishindia zawadi. Shindano ili limeanza leo na litaendelea mpaka Februari 4,2018.  Kuna zawadi nyingi sana kunywa sasa unaweza kuwa wewe ndio mshindi” alieleza Meneja masoko huyo Roselyne Bruno.

Aidha, Pepsi wamemtambulisha mwanamuziki Tekno kama barozi wao wa  Pepsi.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here