TANTRADE yapongeza wananchi kujitokeza kwenye maonyesho ya bidhaa za Tanzania

0
90

Ikiwa imebaki siku moja tu kufikia tamati ya maonyesho ya Bidhaa za viwanda vya Tanzania, Wananchi wameombwa kuendelea kujitokeza kwa wingi kushuhudia maonyesho hayo ambayo yanafikia kilele hapo kesho Desemba 11,2017 katika viwanja vya maonesho saba saba, Barabara ya Kilwa, Jijini Dar es Salaam.

Akielezea  juu ya maonyesho hayo yaliyoanza tangu Desemba 7, mwaka huu,  Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Maendeleo na Biashara Tanzania (TANTRADE) Bw. Edwin Rutageruka, Amepongeza watanzania mbalimbali wanaoendelea kujitokeza kwenye mabanda  hayo ya biashara kwani yamesaidia kuhamasisha hali ya watu kupenda bidhaa zao za ndani ama zile zinazozalishwa na watalaamapamojana viwanda vya  hapa nchini.

“Nawapongeza sana watu wote wanaoendelea kujitokeza kushuhudia maonyesho haya ya bidhaa za viwanda vyetu vya ndani. Inaleta hamasa kubwa kwetu sote na tunaamini Tanzania ya viwanda inazidi kukuwa kwa kasi” alieleza Mkurugenzi huyo wa TANTRADE, Edwin Rutageruka.

Rutageruka amesema kuwa, kuna ongezeko la makampuni kutoka 472 mwaka Jana, hadi kufikia 506 kwa mwaka huu wa 2017.

Aidha, viongozi mbalimbali wameendelea kujitokeza kushuhudia bidhaa hizo wakiwemo Mawaziri, Wakuu wa Mikoa, Wilaya na viongozi wengine wa Kiserikali na mashirika ya Umma na binafsi.

Baadhi ya wananchi walioongea na mtandao huu wamepongeza juhudi za Serikali kwa kuweza kuleta pamoja bidhaa za viwanda vinavyotengenezwa hapa nchini.

Bidhaa mbalimbali za ndani kutoka kwa wazalishaji wakubwa na wadogo wa viwanda vya ndani zinaonyeshwa pamoja na kuuzwa  ikiwemo zile zenye punguzo maalum. Miongoni mwa bidhaa hizo ni pamoja na zile za majumbani, vyakula, vifaa vya ujenzi, vifaa vya maofisini, majumbani, mashule. Pia kuna biadhaa za nafaka kama vile za mazao, vyakula, na bidhaa zingine nyingi.

Na ANDREW CHALE, MO BLOG

moja ya banda la manukato la five star katika maonyesho hayo

Naibu Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji  Mhe. Injinia Stellah Manyanya akieleza jambo kwa kampuni ya AmazingUniforms, alipotembea kampuni hiyo kwenye maonyesho hayo mapema leo Desemba 10,2017,. 

Naibu Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji  Mhe. Injinia Stellah Manyanya akifurahia bidhaa zilizotengenzwa na kampuni ya ndani ya Amazing Uniforms alipotembea kampuni hiyo kwenye maonyesho hayo mapema leo Desemba 10,2017,. 

Naibu Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji  Mhe. Injinia Stellah Manyanya akipata maelezo kutoka kwa Dk. Ibrahim Lyoba Kamrudin alipotembea kampuni ya uwekezaji ya Msagara  katika  maonyesho hayo mapema leo Desemba 10,2017,

Naibu Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji  Mhe. Injinia Stellah Manyanya akisaini kitabu cha wageni alipotembea kampuni ya uwekezaji ya Msagara alipotembelea maonyesho hayo mapema leo Desemba 10,2017,

Naibu Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji  Mhe. Injinia Stellah Manyanya akipata maelezo kutoka kwa msimamizi wa kiwanda cha Urafiki alipotembelea maonyesho hayo mapema leo Desemba 10,2017,

Naibu Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji  Mhe. Injinia Stellah Manyanya akipata maelezo kutoka kwa msimamizi wa kampuni ya Good One, watengenezao bidhaa za malumalu za majumbani wakati alipotembelea maonyesho hayo mapema leo Desemba 10,2017,

 

Mhandisi wa kampuni ya kuendeleza Jotoardhi Tanzania (TGDC), Mhandisi Helena Alfredy (kushoto mwenye bluu) akimwelekeza mmoja wa wananchi waliotembelea banda lao hilo kujua namna kampuni hiyo inavyofanya kazi za utafiti wa umeme utokanao na Jotoardhi.

Mkuu wa mkoa wa Songwe, Luten Mstaafu Chiku Galawa akipata maelezo kutoka kiwanda cha nguo cha Urafiki

Mmoja wa wananchi akipata maelezo kuyoka banda la TBC namna ya wanavyopitisha bidhaa kuwa na ubora

 

Baadhi ya Wakuu wa Wilaya mbalimbali wakimsikiliza mtalaam kutoka Chuo kikuu cha UDSM, wakipata maaelezo namna ya vifaa vya ufundi namna vinavyofanya kazi.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here