MIAKA 20 YA MKESHA MKUBWA KITAIFA – DUA MAALUM

0
163

Kwa nini Dua Maalum 2017/2018 ifanyike Kwa Taifa?

Inaonekana kama msisitizo wa dua hii ya kuliombea Taifa ipo sasa tu, la hasha! Dua hii ipo tangu mwaka 1997 hadi leo. Lakini kwa kuwa imani ni sasa kwa ajili ya baadaye:

(Waebrania 11 : 1),

  1. haiepukiki jambo hili kuonekana ni jipya kila mwaka. Na kwa kuwa adui hata sasa anaendelea kutenda kazi zake, haiwezekani sisi tulio wa Mungu wa kweli, tukanyamaza na kukaa kimya kama watanzamaji tu, tusijibu mashambulizi ya shetani.

Kwa miaka ishirini sasa Watanzania 🇹🇿 wamebarikiwa neema ya kuwa na Dua Maalum kwa Taifa. Kama mdau wa Habari Tanzania tunaomba ushiriki pamoja kuwahabarisha watanzania na marafiki wa Tanzania 🇹🇿 juu ya maeneo mbali mbali utakapofanyika Mkesha Mkubwa Kitaifa – Dua Maalum mwaka 2017/2018.

2 Nyakati 7 : 14

“Ikiwa watu wangu, walioitwa kwa jina langu, watajinyenyekesha, na kuomba, na kunitafuta uso, na kuziacha njia zao mbaya; basi, nitasikia toka mbinguni, na kuwasamehe dhambi yao, na kuiponya nchi yao.”

2 Chronicles 7 : 14

“if My people who are called by My name will humble themselves, and pray and seek My face, and turn from their wicked ways, then I will hear from heaven, and will forgive their sin and heal their land.”

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here