Saida Kaloli kuibuka upya kwenye Tamasha la Sauti za Busara 2018

0
1030

Mwanamuziki Saida Karoli anayeimba nyimbo za asili ya Kihaya nchini anatarajiwa kuamsha upya hisia zake za muziki kupitia tamasha kubwa na pendwa Barani Afrika la Muziki la Afrika Mashariki, Sauti za Busara ambalo linatarajia kufanyika Februari 8-11,2018, Visiwani Zanzibar.

Akuzungumza mbele ya waandishi wa Habari mapema leo Mwanamuziki huyo, ameweza kuishukuru Busara Promotions ambao ni waandaaji wa tamasha la Sauti za Busara linalofanyika kila mwaka visiwani Zanzibar.

Akizungumzia tamasha hilo, Saida Kaloli amebainisha kuwa, kwa sasa anarejea upya kwenye Busara kwani anaamini litamjenga kwa kiwango kikubwa kupitia mziki wake.

“Tamasha la Sauti za busara linatutoa kwenye fikra tofauti kwa kila mmoja wetu. Kila mshiriki anayeenda kushuhudia na msanii anayepata kutumbuiza pia.

..Nasema asante sana kushiriki tamasha la Sauti za Busara. Kwani ushiriki huu ni kujifunza kwa maana ya vyombo na uimbaji. Vilevile ni ujuzi wa kujifunza kile ambacho hatukijui” ameeleza Saida Kaloli mbele ya waandishi wa Habari wakati wa mkutano maalum uliondaliwa na Busara Promotions, tukio lililofanyika Jijini Dar es Salaam, Golden Tulip City Center.

Aidha, Saida Kaloli ameweka wazi kuwa, mashabiki wake wamtegemee kupata vitu vipya jukwaani kwani anaamini ujio wake utakuwa wa hali ya juu ikizingatiwa kuwa na nyimbo mpya ambazo watu watazipenda.

Mbali na Saida Kaloli wasanii wengine watakaopamba tamasha hilo ni pamoja na Zakes Bantwin (Afrika Kusini), Kasai Allstars (DRC), Somi (Uganda/USA), Ribab Fusion (Morocco), Mlimani Park Orchesta (Tanzania), Grace Matata (Tanzania), Segere Original, (Tanzania).

Pia wapo Mohamed Ilyas & Nyota Zameremeta (Zanzibar), Makadem (Kenya), Diana Samkange ‘MaNgwenya’ (Zimbabwe), Fatma Zidan (Misri / Denmark), Inganzo Ngari (Rwanda). Simangavole (Reunion), Maia & the Big Sky (Kenya), Kiltir (Reunion), El Dey (Algeria), Simbin Project (Senegal / Uswisi), CAC Fusion (Tanzania), Mbanaye (Malawi), Ernest Ikwanga (Malawi) na Isack Abeneko (Tanzania) na wengine wengi.

Uongozi wa Busara Promotions umekutana na waandishi wa habari kuzungumzia maandalizi ya tamasha hilo ambalo linatarajiwa kufanyika wiki mbili zijazo katika viunga vya Unguja Mjini Zanzibar.

Na ANDREW CHALE-BONGONEWS.CO.TZ

Mwanamuziki Saida Karoli anayeimba nyimbo za asili ya Kihaya nchini (Kushoto) akipokea kipaza sauti kutoka kwa Mkurugenzi wa Busara Promotions, Yusuf Mahmoud, mapema leo Januari 23,2018.

Mwanamuziki Saida Karoli anayeimba nyimbo za asili ya Kihaya nchini (Kulia) akizungumza na Mwandishi wa Habari wa Gazeti la Mwananchi, Herieth Makweta, mapema leo Januari 23,2018.

Mwanamuziki Saida Karoli anayeimba nyimbo za asili ya Kihaya nchini (Kushoto) akizungumza na waandishi wa Habari (Hawapo pichani) juu ya ujio wake mpya katika tamasha la Sauti za Busara linalotarajiwa kufanyika Februari 8-11,2018,Visiwani Zanzibar. anayemfuatia ni Mkurugenzi wa Busara Promotions, Yusuf Mahmoud, Balozi wa Uswisi nchini Tanzania Bi. Florence Tinguely, Mwenyekiti wa Tamasha la Sauti za Busara, Mheshimiwa. Simai Mohammed Said  mapema leo Januari 23,2018, Jijini Dar es Salaam

Mwanamuziki Saida Karoli anayeimba nyimbo za asili ya Kihaya nchini (wa pili kutoka Kushoto) akiwa katika picha ya pamoja kuonesha Umoja, sambamba na viongozi wa Busara Promotions, pamoja na Mabalozi ambao ni wadau wkubwa katika maendeleo ya tamasha hilo. mapema leo Januari 23,2018, Jijini Dar es Salaam.

(PICHA ZOTE NA ANDREW CHALE-BONGONEWS)

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here