Kumekucha tamasha la Sauti za Busara,ni Februari 8-11 Zanzibar

0
156

Kumekucha macho na masikio yote kuelekezwa Visiwani Zanzibar katika viunga vya Mji Mkongwe wa Unguja ambapo watu kutoka mataifa mbalimbali wanatarajiwa kujumuika pamoja kufurahia muziki safi na wa kuvutia kwenye tamasha la Sauti za Busara, Februari 8-11, 2018.

Waandaaji wa tamasha hilo Busara Promotions wameeleza kuwa, tayari tiketi zimeanza kuuzwa mtandaoni kupitia: Click HERE to Buy Tickets huku tiketi za kawaida kuanza kuuzwa Februari 5, katika mlango wa kuingilia Ngome Kongwe litakapofanyika tamasha hilo.

Akizungumza na waandishi wa Habari Jijini Dar es Salaam katika tukio lililofanyika katika hoteli ya Golden Tulip City Centre, Mkurugenzi wa Busara Promotins ambao ni waandaji wa Tamasha la Sauti za Busara, Yusuf Mahmoud amesema tamasha hilo linatarajiwa kuunganisha watu wa Mataifa yote sehemu mbalimbali.

Kwa mwaka huu tamasha hilo limebeba kauli mbiu ya “Kuunganishwa na Muziki”, Waafrika na wageni kutoka katika kila pembe ya dunia.

Aidha, Yusuf Mahmoud amesema tamasha linaitangaza Zanzibar na Tanzania sehemu mbali mbali duniani kwa kuwa linavutia mapromota wa kimataifa na kutoa fursa adhimu kwa wanamuziki wa Afrika Mashariki kuupeleka mziki wao duniani kote.

“Ndani ya majukwaa matatu kwa siku nne, tamasha litakuwa na maonyesho 46 yenye hadhi ya kimataifa ambayo kwa asilimia 100 yatapigwa mbashara. Tamasha litawaweka pamoja wanamuziki wadogo na wakubwa kutoka katika viunga vyetu na hata nje ya nchi, likibeba dhumuni moja huku tukisimama pamoja kupitia kauli mbiu ya ‘kuunganishwa na muziki”, amesema Yusuf.

Yusuf Mahmoud amesema orodha ndefu ya wasanii watakaoshiriki mwaka huu itakuwa chachu kwa kila mtu atakayefika kujionea tamasha hilo.

Miongoni mwa wasanii hao watakaoshiriki tamasha hilo, akiemo Mwanamuziki wa nyimbo za Asili la kabila la Kihaya, Saida Kaloli na wanamuziki wengine wengi wakiwemo Zakes Bantwini (Afrika Kusini), Kasai Allstars (DRC), Somi (Uganda/USA), Ribab Fusion (Morocco), Kidum na tha boda boda band (Burundi/Kenya), Mlimani Park Orchestra (Tanzani), Grace Matata (Tanzania) na Msafiri Zawose (Tanzania).

Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Tamasha hilo, Said Mohamed amewashukuru wadau wakubwa kuendelea kujitokeza kudhamini tamasha hilo licha ya kujiendesha kwa gharama kubwa huku fedha nyingi wakijaribu kutegemea wadhamini wa kigeni hasa mashirika ya nje na Mabalozi.

NA ANDREW CHALE-BONGONEWS

Mwakilishi wa Balozi wa Norwei hapa nchini, Bi. Annette Pettersen  akizungumza katika tukio hilo

Baadhi ya waandishi wa Habari wakichukua matukio katika tukio hilo la Busara Promotions wakati walipozungumza na waandishi wa Habari Jijini Dar es Salaam.

Mkurugenzi wa Busara Promotions Yusuf Mahmoud akizungumza katika tukio hilo

Poul Owele akizungumza katika tukio hilo wakati wa kukaribisha wanahabari kwenye mkutano huo

Baadhi  ya wadau wakiwa kwenye tukio hilo

Mwenyekiti wa Tamasha la Busara, Mh. Simai Said akihojiwa na Mwandishi wa Nipashe wakati wa tukio hilo

Baadhi ya wageni waalikwa wakibadilishana mawazo wakati wa tukio hilo

Uongozi wa Busara Promotions pamoja na wageni waalikwa wakiwemo Mabalozi na Wasanii wakiwa wameshikana mikono kwa pamoja kama ishara ya Umoja inayoendana na kauli mbiu ya mwaka huu ya tamasha hilo ya: “Kuunganishwa na Muziki”, Waafrika na wageni kutoka katika kila pembe ya dunia.

(PICHA ZOTE NA ANDREW CHALE-BONGONEWS).

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here