Ndoa za Utotoni bado ni tatizo Nchini na Afrika Mashariki

0
174
TATIZO la ndoa za utotoni katika Tanzania na nchi za Afrika Mashariki limeonekana ni tatizo kubwa sana katika maeneo hayo ambapo kitakwimu inaonyesha kuwa kati ya mikoa kumi bora Mkoa wa Shinyanga unaongoza kwa kuwa na asilimia 59 na Mkoa wa Singida umeshika nafasi ya nane kwa kuwa na asilimia 42.
Meneja wa Shirika la kidini lisilokuwa la kiserikali la World Vision Tanzania (WVT) Kanda ya kati,Faraja kulanga aliyasema hayo kwenye uzinduzi wa mpango wa kutokomeza mimba za utotoni uliofanyika katika ukumbi wa mikutano wa Kanisa Katoliki,mjini Singida.
Alifafanua kwamba kwa mujibu wa utafiti uliofanywa na Tanzania Demokratic Health Survey ya mwaka 2010 inaonyesha kitakwimu kwamba tatizo la ndoa za utotoni,Mkoa unaoongoza ni Mkoa wa Shinyanga wenye asilimia 59 huku Mkoa wa Singida ukiwa na assilimia 42 na hivyo kushika nafasi ya nane katika mikoa hiyo kumi bora.
“Kwa maana kwamba ule utafiti huwa unakwenda kuuliza kila nyumba na wakiuliza katika kila nyumba mama alipata ujauzito katika umri gani,wale waliopata mimba katika umri chini ya miaka 18 ilikuwa ni asilimia 59.”alifafanua Kulanga.
Kwa mujibu wa Meneja huyo katika asilimia 42 ya familia zilizoulizwa kina mama kwamba alipata ujauzito akiwa na umri chini ya miaka 18,asilimia 42 wakaonekana ilikuwepo na kwamba shirika hilo lilifanya utafiti katika Kanda saba kwenye maeneo wanayofanya kazi.
Aidha Meneja huyo aliweka bayana kwamba kanda hiyo ina jumla ya kanda saba ambazo ni pamoja na Kanda ya Pwani ambayo ndiyo inayoongoza ikifuatiwa na kanda ya kati ambayo ni pamoja na Mkoa wa Singida ambapo kitakwimu inaonyesha kuwa kuna tatizo kubwa la ndoa za utotoni.
Kwa upande wake Afisa wa dawati la jinsia na Watoto kutoka jeshi la polisi wilaya ya Singida,Amina Fakih Abdallah alibainisha kuwa kinachochangia kwa namna moja au nyingine kuwepo kwa ongezeko la mimba za utotoni ni ukinzani wa sheria zinazosimamia mimba za utotoni.
Hata hivyo afisa huyo wa dawati la jinsia na watoto alisisitiza pia kwamba katika sheria zinazosimamia ndoa hizo za utotoni,hakuna sheria iliyosimama na inayolinda mimba za utotoni kutokana na moja ya sheria hizo kuruhusu mtoto aolewe akiwa na umri wa miaka 14 huku sheria ya jinai inakataza motto mwenye umri wa miaka 18 kuolewa.
“Sasa kama inalinda mimba za utotoni kuna sheria inaruhusu mtoto wa kike aolewe akiwa na umri wa miaka 14,sasa hii sheria inaporuhusu mtoto aolewe akiwa na umri wa miaka 14,we huku kwenye sheria ya jinai unasema kwamba huyu mtoto aliye chini ya miaka 18 haruhusiwi kuolewa”alifafanua.
Naye Mkuu wa wilaya ya Singida,Eliasi Tarimo akizindua Mpango wa mapambano dhidi ya kutokomeza ndoa za utotoni za mradi wa Mtinko ADP uliopo wilaya ya Singida alisisitiza pia juu ya kuondoa mapungufu yaliyopo katika sheria zinazosimamia mimba za utotoni ili ziweze kufanana badala ya kuendelea kukinzani.
Kwa mujibu wa Tarimo ambaye pia ni Mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na usalama katika wilaya hiyo sheria zote hizo hazina budi kutamka bayana kwamba umri wa motto usizidi miaka 18,ikiwemo sheria ya ndoa,sheria ya motto mwenyewe na kipengere kinachotamka kuwa motto anaweza kuolewa kwa kibali cha wazazi.
Na,Jumbe Ismailly SINGIDA

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here