Wadau watoa neno kwa viongozi wa Serikali wanaoshtukiza Bandari Dar

0
238

Wadau wa Bandari nchini wamesema ziara za mara kwa mara za viongozi bandarino sio suluhisho la kuimarisha ufanisi katika eneo hilo bali kinachohitajika nikuweka watu wenye taaluma na masuala ya bandari.

Wamesema shughuli za bandari ni Sayansi hivyo lazima wapatikanike watalaamu ambao wanajuwa namna ya kuendesha bandari lakini sio ziara za mara kwa mara zinazofanywa na Viongozi japo nazo kwa kiasi flani zinasaidia.

Wadau hao wa Bandari wametoa ushauri huo kupitia kituo kimoja cha Luninga  hapa nchini ambacho kilirush mubashara matangazo yake katika kipindi Cha saa moja cha kipima joto.

Akizungumza katika kipindi hicho mshauri na mtalamu wa mambo ya Bandari Julius Mhurunga alisema hakuna namna nilazima eneo hilo liongozwe na watalamu.

Alisema pia inatakiwa kuwepo kwa watu wautafiti wa mambo ya bandari kama ilivyo katika mataifa mengine, napia lazima pawepo na mafunzo ya kitalaamu kwa vijana wetu.

“Nimejaribu mara kadhaa kutoa ushauri wangu kwa maandishi kwa maana ushauri wanamna gani mambo yanatakiwa yaendeshwe katika eneo zima la Bandari lakini hadi leo hakuna majibu ila najuwa ipo siku watajibu.

Aliongeza kuwa yeye kama mtalaamu anatumia utalamu wake kufundisha watu wengine huku akitolea mfano kuwa amefundisha vijana Uiengera, Kanya na mapema mwezi huu anakwenda Afrika kusini.

“Unajuwa  suluhisho  la kufanya viongozi wasifike bandarini nikuwa na watalaamu wa kufanya shughuli za bandari ambao watapewa mafunzo kabisa. Bandari ni sayansi. “alisema Mhurunga.

Kwaupande wake Rais wa Wakala wa Forodha Bandarini hapo Stephen Ngatunga akizungumzia vitendo vya wizi vinavyofanyika bandarini alisema vinatokana na watu wachache ambao si waaminifu.

“Sisi hatuhusiki kuangalia kwenye meli kuna nini mara nyingi tunadili na makalatasi (Document) hivyo kuhusu mzigo mara nyingi mwenye mzigo ndio anahusika sana. ” alisema Ngatunga

Pia alisema ziara za viongozi hao sio mbaya ila kinachohitajika niuboreshaji wa miundombinu  ya bandari hasa katika kipindi hiki ambacho baadhi ya maeneo wanaboresha bandari zao.

Alisema hivi sasa nchi karibu nane ukanda huu wa Afrika zinategemea bandari ya Tanzania kwa hiyo hapo ndio pakuboresha bandari ili kuleta ufanisi zaidi ambapo kutachochea meli nyingi kuingia nchini.

Ashraf Kani yeye ni Mwenyekiti wa Bandari kavu akichangia katika kipindi hicho alisema hivi sasa hali ya bandari si mbaya Kwan makontena yanakuja kwa wingi ambapo alidai hadi kufika mwaka 2020  bandari itakuwa nauwezo wa kushusha kontena milioni moja ukilinganisha na sasa kontena laki tano.

Pia akizungumzia ziara za viongozi alisema zinatija na zimesaidia kuimarisha hali ya bandari huku akisisitiza umuhimu wa bandarini kavu.

Hata hivyo Wananchi waliopiga simu studioni walisema ziara za viongozi zinapaswa kuendelea kwasababu watendaji hao hawana uzalendo na nchi yao na kikubwa wanajali maslahi yao huku wakitaka usalama wa taifa utumike zaidi kumpeleka taarifa Rais. John Magufuli.

NA MWANDISHI WETU-BONGONEWS

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here