Mawaziri wa Maliasili na Mazingira wa EAC wafanya mkutano Jijini Arusha

0
81
Mawaziri wa Maliasili na Mazingira kutoka nchi za Afrika Mashariki mapema leo Februari 9,2018, wamekutana Jijini Arusha katika mkutano maalum wa tano wa Baraza la Kisekta la Mawaziri wa Maliasili na Mazingira wa Nchi hizo katika ukumbi wa EAC jijini Arusha.
Mkutano huo ulilenga kujadili na kusaini makubaliano mbalimbali ya namna bora ya kusimamia sekta hizo katika nchi wanachama.
Miongoni mwa Mawaziri hao  kwa Tanzania, Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla aliweza kushiriki mkutano huo akiungana na Mawaziri wengine akiwemo Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira, January Makamba.
 Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira, January Makamba (kulia) akisaini baadhi ya makubaliano yaliyofikiwa katika mkutano wa tano wa Baraza la Kisekta la Mawaziri wa Maliasili na Mazingira wa Nchi za Jumuiya ya Afrika ya Mashariki uliohitimishwa leo katika ukumbi wa EAC jijini Arusha. Mkutano huo ulilenga kujadili na kusaini makubaliano mbalimbali ya namna bora ya kusimamia sekta hizo katika nchi wanachama. Wanaoshuhudia ni Mawaziri wa Mazingira kutoka Uganda na Kenya.
 Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla (kulia), Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira, January Makamba (wa pili kulia) na Balozi wa Sweden nchini Tanzania, Bi. Katerina Rangnitt wakiangalia baadhi ya michoro ya katuni za kuhamasisha uhifadhi wa mazingira muda mfupi baada mkutano wa tano wa Baraza la Kisekta la Mawaziri wa Maliasili na Mazingira wa Nchi za Jumuiya ya Afrika ya Mashariki uliohitimishwa leo katika ukumbi wa EAC jijini Arusha. Mradi huo ya katuni unafadhiliwa na Serikali ya Sweden kwa ushirikiano na Serikali ya Tanzania.
 Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla (kulia) na Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira, January Makamba wakimsikiliza mmoja ya wachora katuni za kuhamasisha uhifadhi wa mazingira muda mfupi baada mkutano wa tano wa Baraza la Kisekta la Mawaziri wa Maliasili na Mazingira wa Nchi za Jumuiya ya Afrika ya Mashariki uliohitimishwa leo katika ukumbi wa EAC jijini Arusha. Mkutano huo ulilenga kujadili na kusaini makubaliano mbalimbali ya namna bora ya kusimamia sekta hizo katika nchi wanachama. 
 Picha ya pamoja ya baadhi ya wajumbe wa mkutano huo.
(PICHA ZOTE NA HAMZA TEMBA-WMU)

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here